Paul Makonda Aanza Kazi Kama Mkuu wa Mkoa...Atoa Agizo Kwa Wakuu wa Idara za Halmashauri Kumfikishia Ripoti Jinsi Walivyojipanga Ndani ya Masaa 24

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewagiza wakuu wa idara wa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam kutoa ripoti za matatizo ya wananchi na jinsi walivyojipanga ndani ya masaa 24.
Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri hizo ikiwa ni siku ya kwanza kuingia katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya kuapishwa jana, Makonda amesema wananchi wa Dar es Salaam wanakabiliwa na changamoto za ulinzi,maji,biashara pamoja na elimu  hivyo lazima matatizo hayo yapate ufumbuzi katika kusaidia wananchi kuondokana na changamoto hizo.

Makonda amesema kuwa kwa muda alioutoa wa masaa 24 ni mkubwa hivyo lazima wafanye kazi hiyo jinsi walivyojipanga katika kutatua changamoto hizo.
Amesema wakati umefika katika kuwatumikia wananchi kuwaondolea  kero zao ambazo zinafanya kuwa na malalamiko yasioisha.

Makonda amesema amekutana na Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuzungumzanaye juu ya suala la ulinzi na usalama  kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa kukutana huko sio mara ya kwanza ataendelea ikiwa ni lengo la kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua kero zao.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Paul Makonda... Mwanzo Ni nzuri Na nia inadhihirisha kuwa Ni njena Na usongo WA kuwajibika unao.. Nilichoona labda kingekuwe Kama nyongeza kuondoa red tape.. Ni tel ya mawasiliano yako au mwakilishi wako ambacho dogo Na kubwa linafoka Na mpango wa utatuzi with time frame unawekwa ukipita unaescalete kwa wizara husika Na ikiahindwa JPJM anahuaishwa kutoa ufumbuzi... JPJM tunae Na Ni mwajibbikaji alipita kiasi cha natakwa. Unanielewa Paul.. Nakutakia kazi njena Na ubunifu wa manufaa kwwtu sote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad