Paul Makonda Aweka Wazi Mikakati yake ya Kuubadilisha Mkoa wa Dar es Salaam, Ataka Wenye Nyumba zilizochakaa Wazipake Rangi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezindua kampeni ya kufanya jiji la Dar es salaam kuonekana safi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko pamoja na kufanya jiji kuwa kivutio kwa wageni.

Makonda amefanya uzinduzi huo leo alipokuwa akizungumza na watendaji wa halmashauri zote za Dar es salaam katika kuwakumbusha namna ambavyo amejipanga katika kutatua kero za wananchi na kuwataka watendaji hao kuendana na kasi yake.

Kampeni hiyo ambayo inakwenda kwa jina la 'Naona Aibu' ina lenga kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi kuanzia kwenye mazingira ya majumbani hadi kwenye barabara zote za jiji.
''Hatuwezi kuwa wasafi wa mioyo kama tunaishi kwenye mazingira machafu kila mtu aseme naona aibu, ukipanda kwenye daladala ukiona uchafu sema naona aibu, ukiwa mtaani kwako sema naona aibu''. Amesisitiza Makonda katika hotuba yake ambayo imedumu kwa zaidi ya saa 3.

katika kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa, ametangaza kuanzisha shindano kwa kila mtaa, ambapo mitaa yote ya jiji la Dar es salaam itashindanishwa kwa usafi, na mtaa utakaoibuka mshindi utapata zawadi ikiwa ni pamoja na kitita cha shilingi milioni 5 kwa wajumbe wa mtaa huu.

Pia amewashauri wenyeviti wa serikali za mitaa kuwahamasisha wananchi wao kupaka rangi nyumba zao ili kupendezesha jiji kwa kuwa usafi ni pamoja na kuwa na nyumba zinazopendeza.
"Usafi ni pamoja na kupendezesha nyumba, waambieni watu wenu wapake rangi nyumba zao, zipendeze" Amesema mkuu huyo wa mkoa.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amewataka watendaji wote wa mkoa wa Dar es salaam na wanasiasa wote kutambua kwamba muda wa siasa sasa umekwisha na kilichobakia ni kufanya kazi kwa maendeleo ya wananchi.

''Wanasiasa kwenye jambo langu ukikaa mbele nitakushughulikia na wala sioni haya''- Amesema Makonda.
Hata hivyo amepiga marufuku biashara mbalimbali zinazofanyika katika maeneo ya barabara za jiji la Dar es salaam na kusisitiza kuwa biashara hizo hulikosesha taifa mapato vilevile kuweka wananchi katika hali ya hatari ya kugongwa na magari muda wowote.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vibanda vyote vya pembeni mwa barabara vinafichsha wahalifu

    ReplyDelete
  2. walipe hela ya kaupakia rangi, kwani unafikiri mtu hapendi tu nyuma yake iwe nzuri, hela ya kula hana then una mwambia apeke nyuma rangi, fikiria kabla ya kuropoka.

    ReplyDelete
  3. Wewe ndie unaeropoka kumiliki nyumba dar usiwe na uwezo wa kupaka rangi labda uwe mchafu koga ndio wale wenye kuweni vibanda kiza na mapira ya magari chakavu kwenye kona badala ya gardens tujifunze umaridadi sio kuoga na mikorogo

    ReplyDelete
  4. baba tengeneza kwanza miundombinu huku chobingo vijumba havijapimiwa ramani wala uwanja aipake rangi then lukuvi aje aibomoe hati zenyewe xhida., uongozi mgumu jamani mwe!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad