Mkali wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke ‘Davido’, amedai kwamba kutokukamatwa kwake na polisi kumetokana na mashabiki wake.
Wiki iliyopita, Davido alikuwa kwenye nyumba yake nchini Marekani, lakini polisi walikuwa na wasi wasi na msanii huyo kumiliki nyumba hiyo kwa kuwa walikuwa hawamjui kama yeye ni msanii.
“Niwe muwazi, mashabiki wangu wamenisaidia baada ya kukamatwa na polisi kwa sababu namiliki nyumba ya thamani kubwa wakitaka kufahamu ninakopata fedha.
“Ilikuwa ngumu kunielewa lakini walikuja kukubali baada ya kuwaonyesha idadi kubwa ya mashabiki zaidi ya milioni 100 wanaofuatilia kazi zangu kupitia mtandao wa ‘You Tube’.
“Nawashukuru sana mashabiki wangu nawapenda sana na nitaendelea kuwapenda katika maisha yangu,” aliandika Davido kwenye mtandao wa Instagram.
Huo uongo wa kinaijeria kawadanganye wanaijeria wenzako na baadhi ya waafrika wasioijua Marekani!! Polisi wa huku USA hawafanyi kazi za kubabaisha,kuwa na nyumba kubwa na nzuri hiyo haiwausu ( Sio kazi yao!!) Mashabiki wako hakuna walicho kusaidia, kama nyumba yako ni ya halali usiwe na wasiwasi, kama kweli unayo nyumba na sio ya halali ngoja tuone kama hao washabiki wako watakusaidia. PS Ukitaka kuona nyumba kubwa na nzuri hapa USA kawatembelee wahya kutoka Tanzania utashangaa!!
ReplyDeletenyie udaku hamna habari mpya za kuandika mbona hii habari ilitoka mda mrefu sana uliopita halafu mnarudia tena kutuwekea hapa kama hamna habari mpya ni heri mkae kimya maana inaboa sana
ReplyDelete