Prof. Beno Ndulu: Watu Wanaongea Wasiyoyajua, BOT Haina Wafanyakazi Hewa

Hatimaye gavana wa BOT Prof. Beno Ndulu ametoa majibu kwa rais John Magufuli huku akisisitiza kuwa watu wanaongea wasiyoyajua na kuomba apewe majina pamoja na taarifa za wale watu wanaodhani kuwa ni wafanyakazi wasio na umuhimu BoT.

Hayo yanajiri siku moja baada ya rais John Magufuli kumuagiza gavana huyo kuwaondoa ndani ya utumishi wa BoT wafanyakazi wote wasio na umuhimu pamoja na wale wanaojulikana kuwa ni wafanyakazi hewa.

Jana gavana akiongea na vyombo vya habari pamoja na gazeti la MTANZANIA alisema kuwa kila mfanyakazi wa BoT ana umuhimu wake huku akisisitiza kuwa watu wanaongea wasiyoyajua. Prof. Ndulu pia alisisitiza kuwa yule anayedhani kuwa kuna wafanyakazi wasio na umuhimu BoT basi ampelekee majina yao pamoja na taarifa zao!

Hata hivyo gavana huyo aliweka wazi kuwa rais ametoa agizo hivyo ni muhimu kuzingatia agizo la rais lakini akaweka mkazo kuwa BoT itajiridhisha kwa kina kwanza kabla ya kuchukua hatua yoyote ile!

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. a












    safi sana prof...


    ReplyDelete
  2. Wewe ndulu ni jipu subiri muda wako,unatetea ujinga?

    ReplyDelete
  3. Prof ndulu baba hii siyo serikali ya kulindana uwe na uhakika na unachokisema.

    ReplyDelete
  4. anamtafuta JPM huyu, nadhani bado hajamjua sawasawa! anafikiri ni yule wakuchekacheka!! HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  5. Huyu Baba alishindwa hata kumjibu Rais swali aliloulizwa wakati wako pamoja na tena mbele ya Kamera sasa hivi ndio ameamka na mzimu wake kujibu yale aliyoyashindwa wakati alipoulizwa na Rais, kwa kweli huyu si aina ya kiongozi anayefaa hasa kuongoza taasisi kubwa na inayotakiwa kuilinda hazina ya Taifa letu.......huyu ni jipu linalotakiwa kutumbuliwa mara moja na tena bila ya aibu na haya ndio matokeo ya kukaa muda mrefu kwenye madaraka mpaka kufikia kujisahau.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad