Roma Asema Hapendi Kumpost Mpenzi Wake Kwenye Mitandao ya Kijamii..Sababu Hii Hapa..

Msanii wa Hip Hop Tanzania,Roma amefunguka kuwa huwa hapendi kumpost mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii kwa kuhofia kuwa inaweza kumharibia biashara yake muziki.

Roma anaamini kuwa kuna mashabiki wengi na kila mtu anapenda kitu fulani kutoka kwa msanii sio nyimbo tu,wengine hata kukupenda kimapenzi kwa hiyo kumpost mpenzi wako kila mara inaweza kuwafukuza mashabiki wa namna hiyo.

“Sometimes kumpost sana unaharibu biashara yako hasa hii ya sanaa yetu,mashabiki wanakuja kwenye show yako sio tu kwa sababu ya ngoma zako,kila mtu anachokipenda kwako...” alisema Roma ambaye amewahi kumpost mpenzi wake mara moja toka ajiunge instagram.

Source:Fredrick Bundala,conversation with Roma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad