Baada ya timu ya taifa ya Chad kujitoa kwenye mashindano ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za AFCON mwaka 2017, watu wengi wamekuwa na maoni tofauti hususan nafasi ya Tanzania kufuzu kwa fainali hizo ambazo zitafanyika nchini Gabon.
Mchambuzi wa masuala ya michezo Shaffif Dauda kutoka Clouds Media Group yeye ametoa maoni yake juu ya kujitoa kwa Chad huku akieleza athari itakayozipata timu ambazo zilikuwa kundi moja na Chad kutokana na timu hiyo kujitoa kwenye mashindano pamoja na nafasi ya Tanzania kufuzu kwenye mahindano hayo makubwa barani Afrika kwa ngazi ya timu za taifa.
Athari kwa timu za kundi G baada ya Chad kujitoa
“Athari ya kwanza kwa Chad kujitoa ni kwa timu zote ambazo zilikuwa kundi moja na Chad kwa maana ya Tanzania, Misri na Nigeria. Kwenye kundi hili, timu tatu ndizo ambazo zilionekana zinapigania nafasi yna kufuzu kwa fainali za AFCON zitakazofanyika Gabon, walitegemea Chad awe kama ‘punching bag’ kwa timu zote ili zijekuviziana zenyewe kwa zenyewe”.
“Ukiangalia hili ili kuthibitisha kauli yangu, Tanzania tayari alishampiga Chad nyumani kwao na kuchukua pointi tatu, Nigeria alishachukua poini tatu nyumbani kwa Chad na Misri tayari naye alishampiga Chad na kuchukua pointi tatu”.
“Sasa kinachotokea ni kwamba, kujiondoa kwa Chad kwenye mashindano haya kunaathiri timu zote kwa maana ya pointi zote ambazo timu tatu zilishazivuna mbele ya Chad zinafutika na michezo mingine ambayo ilikuwa inafuatia inafutika”.
“Kwahiyo kwenye msimamo wanaangalia matokeo ya timu tatu zinazobaki kwenye mashindano kwa maana hiyo, Tanzania badala ya kuwa na pointi 4 itabaki na pointi yake 1 na zile pointi 3 ambazo zilikuwa zinahesabiwa zinafutwa, kwa maana kama Tanzania ingeshinda dhidi ya Chad kwenye mchezo wake wa marudiano ingeendelea kutengeneza mazingira chanya ya kufuzu kwenye mashindano yajayo ya AFCON yanakuwa yamepotea”.
Nafasi ya Tanzania kufuzu kwenye fainali za AFCON 2017
“Kilichobaki kwa sasa ni kuona kwa namna gani Tanzania katika mechi mbili zilizosalia dhidi ya Misri na Nigeria wataweza kujitutumua na kufikisha idadi ya pointi ambazo timu hizo zitashindwa kuzifikisha ili Tanzania iweze kufuzu ikiwa kinara wa kundi G”.
“Kwa harakaharaka ukiangalia baada ya kuyafuta matokeo ya Chad, anayenufaika ni Misri ambaye anabaki na pointi nne ambazo alizipata dhidi Tanzania na Nigeria. Kwahiyo mechi inayokuja kati ya Misri dhidi ya Nigeria, kama Misri itashinda mchezo wake moja kwa moja inakuwa imekata tiketi ya kufuzu kwa fainali zijazo kwa kufikisha pointi 7 na kutengeneza mazingira mazuri”.
Nafasi ya best loser kutoka kundi G
“Nashindwa kulizungumzia hili moja kwa moja kwasababu sijajua CAF watafanyaje, ni vigumu kumpata best loser kwenye kundi hili kwasababu kupata best loser wanaangalia timu ya pili iliyofanya vizuri kwenye kundi lenye timu nne.
“Lakini kama hili kundi lingekuwa na timu tatu toka mwanzoni wakati makundi yanapangwa, kundi ambalo huwa lina timu tatu mara zote halihusishwi kwenye mchakato wa kumpata best loser”.
SOMA Mtazamo wa Mchambuzi Shaffih Dauda Baada ya Chad Kujitoa Kuwania Kufuzu Fainali za AFCON 2017
0
March 28, 2016
Tags