Steve R&B Ataja Hiki Kama Kikwazo cha Bongo Fleva Kuwika Kimataifa...Kipi Hicho?

Msanii wa bongo fleva toka Tanzania Steve RnB ametaja uchache wa wasanii wa bongo fleva wanaopeperusha bendera ya Tanzania kimataifa ndio sababu kubwa inayofanya muziki huo usitambe sana nje ya mipaka.

Steve amesema kuwa ametembelea nchi kadhaa ambapo amegundua watu wanasikiliza sana wanaigeria kuliko mziki wetu kwa kuwa wao wana wasanii wengi wa kimataifa na kuongeza wengi hudhani hata Diamond ni Mnigeria.

“Naona muziki wetu kama bado,ila nigeria wamejitahidi..nilikuwa Jamaica wanasikiliza sana wanaigeria .may be wakiwepo watu watano kama Diamond,tunaweza kupiga hatua,kwa sababu tatizo la muziki wetu hatuna watu wengi ambao wanapeperusha bendera..wakati mwingine watu hudhani Diamond ni mnigeria” alisema Steve RnB.

Source: Clouds

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU"Hicho kinachoendelea sio tu kwenu nyinyi wana bongo Flava bali sehemu nyingi tu Bongo Movies pia hivyo hivyo acheni zile roho za"kwa nini"hazina mpango na pia muache au mpunguze "nyodo"na "shobo"pia muache hiyo system ya kikoloni ya"devide and rule"

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad