Tazama Hapa Video ya Goli la Mbwana Samatta Alilopachika Katika Mechi ya leo Kati ya KRC Genk na Oastende

Kwa mara ya kwanza klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambayo inaongozwa na kocha lakini inachezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta, imempa nafasi ya kuanza katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya KV Oastende.

Samatta amepata nafasi hiyo ya kuanza mchezo wa leo March 13, ikiwa ni zaidi ya mechi nne amekuwa akiichezea timu hiyo akitokea benchi. Baada ya Samatta kuanza first eleven, alipachika  goli la kwanza kwa timu yake dakika ya 25 ya mchezo, lakini hilo pia ni goli lake la pili toka ajiunge na KRC Genk.

Samatta Mbwana Ally forward of Krc Genk looks behind him during the Jupiler Pro League match between Royal Mouscron Peruwelz and KRC Genk in the Le Canonnier Stadium in Mouscron, Belgium. *** MOUSCRON, BELGIUM - 06/02/2016  Photo by Nico Vereecken / Photonews ***

Goli la Samatta lilifuatiwa na neema kwa KRC Genk, kuibuka na ushidi wa goli 4-1, magoli ya KRC Genk yalifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 25, Balley dakika ya 39, Pozuelo dakika ya 81 na Camargo dakika ya 88, wakati goli la kufutia machozi kwa KV Oostende lilifungwa na Siani dakika ya 90.

Video ya goli la Samatta

Chanzo:Millard Ayo
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi Mbwana samatta nasisi tunatangazwa Tanzania safi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad