Tungeshangilia Filamu za Bongo Kama Tulivyofanya Kwa Ray na Hadithi yake ya Maji na Weupe Wake, Tungekuwa Mbali

Ray alitengeneza headlines sana hivi karibuni kwa kauli yake kuwa weupe wake umetokana na kunywa maji mengi. Story ilikuwa viral na ilisambaa kwenye mitandao yote.

Watu walianza kupost picha wakinywa maji kuutafuta weupe kama wa Ray kama njia ya kumtania kwa kauli yake hiyo. Sikumbuki mara ya mwisho ni lini muigizaji huyu alikuwa gumzo kama hivi. Hadi kuna tetesi kuwa kutokana na kauli yake kusambaa kwa ukubwa usioelezeka, makampuni ya maji yanataka yampe mchongo.

Hatua hiyo ilinifanya nianze kujiuliza maswali mengi. Ni lini Ray amekuwa midomoni kwa watu kwa filamu aliyoifanya? Ni kwasababu Ray ana filamu yake mpya iitwayo Tajiri Mfupi ambayo ajabu haizungumzwi kama inavyozungumzwa kauli yake hiyo ya maji na weupe wake.

Utasema kuwa filamu za Bongo sio nzuri ama hazina viwango kama za nje lakini kumbe tunawafahamu waigizaji hawa na tunawafuatilia. Tunapenda kujua maisha yao lakini hatupendi kuangalia filamu wanazofanya.

Kwahiyo huenda wachawi wa filamu za Tanzania ambazo zinadaiwa kuanza kudoda, ni sisi wenyewe. Tunafawahamu sana wasanii hawa lakini hatutaki kuunga mkono kazi zao.

Pale wanapotoa kauli za kama za weupe kusababishwa na kunywa maji mengi tunapagawa! Vipi kama tungekuwa na mwamko kama huu wa kusambaza filamu wanazotoa akina Ray? Nadhani tungesaidia kuinyanyua tasnia hii inayopumulia mashine.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unashangaa nini?kila mjadala unaoongelewa sana iwe ni wasanii au jambo lolote ni nyie waandishi wa habari ndio mnasababisha,mnagonganisha na kuchanganya habari za huku na kule ili mradi tu watu wajadili,kwa nini kwa haya uliyoyazungumzia hapo juu usianze kuchanganya kama mnavyochanya umbea,udaku,uone kama halitafanyiwa kama unavyotaka?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahahahahahah!Hasira?

      Delete
  2. me filamu ya bongo mingi mibayaa

    ReplyDelete
  3. kidogo siri ya mtungu ina uhalisia lkn izo nyingine hamna kitu

    ReplyDelete
  4. Sitazami michezo hii mimi nina familia yangu yani.nimeamua kuacha sababu.za scene chafu ukosefu wa adabu tu...hata majimbo ya siku hizi baadhi ni ukosefu wa adabu maneno machafu wanazidi tu kubomoa vijana na watoto wetu aibu kubwa.wanaiga mambo ya kizungu wale mila zao nyinyi mila zenu.nchi yetu ilibarikiwa na adabu heshima stara...sasa inaharibiwa mnategemea ukimwi utaisha vipi na vishawishi hivi.mtu huwezi kutazama mchezo wa kiswahili uchafu mtupu matendo uchafu ndo mnaita nini mumevuta hatua au ndo maendeleo.jamani tujirekebishe kumbukeni kuna watoto...watoto wanaiga mnatuharibiaaaaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad