Upendo Kwa Wasanii Wetu Unapoanza Kuwa Kero Kwa Wasanii wa Nje!

Mitandao ya kijamii imesababisha mashabiki wawe na access ya moja kwa moja na wasanii wanaowapenda.

Imewasaidia kufuatilia maisha yao na kazi zao kwa ukaribu zaidi. Imewasaidia kuwapongeza wanapofanya vizuri, kuwashauri wanapoteleza, kuwakosoa wanapozingua na wengine kuitumia vibaya kwwa kuwatukana wale wasiowapenda. Kikubwa ni kwamba shabiki sasa ana full access katika career ya msanii.

Kupitia mitandao ya kijamii, vita vya kishabiki vimepata uwanja wa kupigania na hicho ni kitu kinachoendelea kila siku. Lakini vipi pale ambapo mapenzi kwa wasanii wetu kwenye mitandao hiyo yanapogeuka kuwa kero kwa wengine?

Mfano mzuri ni kile kinachoendelea kwa wasanii/mastaa aliopiga nao picha Diamond akiwa Marekani. Bahati tu ni kuwa Kanye West hayupo Instagram, kama angekuwepo, huenda sasa angekuwa ameshajua maneno machache ya Kiswahili kutokana na mvua ya comments kutoka kwa mashabiki wa Diamond.

Lakini mtu mwenye experience hii, ni staa wa Empire, Bryshere Y. Gray maarufu kama Hakeem kwenye tamthilia hiyo. Kimuziki pia dogo huyo anajulikana kwa jina la Yazz. Tangu Diamond apost akiwa naye, page yake imevamiwa na waswahili waliokesha wakipiga soga za hapa na pale.

Wametengeneza makao ya muda kwenye page ya Mmarekani huyu ambaye huenda akalazimika kutafuta mkarimani wa Kiswahili ili kumsaidia kung’amua mawili matatu yanayojadiliwa na mashabiki wa kibongo. Wakati mwingine nahisi upendo huu tulionao kwa wasanii wetu unaanza kuwa kero kwa wasanii wa nje.

Nafahamu kuwa hivi bado ni vitu vigeni na itachukua muda kuvizoea (wasanii wa Bongo kufanya collabo na wasanii wakubwa wa Marekani), lakini nadhani ni muhimu tukaendelea kuonesha upendo kwa wasanii wetu, lakini kutowaharibia siku wengine.

Sidhani kama comments zaidi ya 1,000 za Kiswahili ni kitu kinachomfurahisha staa asiyekielewa. Nimesoma baadhi ya comments zinadai kuwa Yazz alimfollow Diamond lakini baadaye akamunfollow tena na wengine wanadhani ni sababu ya fujo alizofanyiwa na mashabiki wake.

Kama ni kweli hiyo ni sababu, basi kumbe mapenzi yetu kwa wasanii wetu yakizidi sana kiasi cha kuzivamia page za wasanii wa nje tukidhani tunataka wajue tunavyowapenda, yanaweza kuwaharibia uhusiano wao.

Wao wataogopa tu kuwaambia mashabiki ukweli huu lakini sometimes wangependa kuona mashabiki wao wana behave kidogo! Sijasahau pia kuwa Jesse “Corparal” Wilson, co-producer wa collabo ya Diamond na Ne-Yo, naye anachezea mvua ya comments za Kiswahili.

Tupunguze mzuka kidogo

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jifunzeni kiingereza,ras simba si yupo.

    ReplyDelete
  2. Sasa kamu unfollow yann ye kama haelewi amuulize domo hebu nisaidie bro washabiki wako hspa wanasema nn..aambiwe asijitie kudharau shabiki ni shabiki tu haijalishi anajua kingereza au hajui...cha muhimu msanii ampende shabiki yake maana bila shabaki hakuna msanii...so huyo hakeem apeleke ujinga huko...domo ni wetu na akiwa na mtu yoyote anayemsapoti nasi tuna toa sapoti kwa wote...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad