Wakati ambapo Austria, Uholanzi na Uingereza zimeshika nafasi ya kwanza katika nchi aminifu duniani, Tanzania na Morocco ambazo ubora wa taasisi zake ulibainika kuwa wa chini, zilifanya vibaya.
Utafiti huo ulifanywa na chuo kikuu cha Nottingham na kuhusisha nchi 159.
Walitumia taarifa zilizopo kuanzia mwaka 2003 za utapeli kisiasa, ukwepaji kodi na rushwa.
Utafiti huo ulibaini kuwa watu wanaoshi kwenye nchi zenye matukio machache ya uvunjaji sheria, walikutwa na uwezekano mdogo wa kudanganya ili kupata fedha ukilinganisha na nchi zenye matatizo ya rushwa.
Ulidai kuwa uwepo wa matukio ya uvunjaji sheria, huwafanya watu kupindisha ukweli.
poland ni kweli kabisa
ReplyDeleteTanzania ni kweli kabisa.
ReplyDeleteHizo list za hao sio wakweli disthonest ni kweli kabisa. Tena wana bla bla nyingi kamba ndefu za uongo uongo
ReplyDeleteHawa wanaotoa utafiti duniani hakuna siku moja nchi ya Afrika au Asia,au Latini Amerika inashinda kwa mambo mazuri.je Watafiti hao wanauraia wa wapi?
ReplyDeleteYaani Italy imekuwa nchi yenye Uaminifu?(hawa Mafia wako wapi?)semeni ukweli
ReplyDeleteitaly ni nchi ambayo watu wanaopenda sana waafrika kuliko nchi nyingine duniani na ndiyo maana iko kwenye list ya most honest mimi ni mwafrika na nilishawahi kufika italy, hata kama italy kuna mafia ni watu wachache sana sio wengi kama Tanzania, na poland ndiyo usiseme mimi ni watu matapeli ile mbaya tena wanastahili kwenye ile orodha ya watu least honest mimi ni mpangaji naishi ulaya mwenye nyumba ni mpoland amenidhurumu sana kwa muda huu nimeishi hapa nitahama muda si mrefu maana mwenye nyumba ana tamaa ya hela kama wabongo
ReplyDeleteKwa hiyo unamaana kuwapenda waafrika ndio uaminifu yaani UKIWA HUELEWANI NA MPOLAND ANAKUWA sio mwaminifu.LUGHA NDIO MUHIMU KUFAHAMU.Kifupi tu Uaminifu ni kutokuwa na hiyana.hauletwi na Taifa unaletwa na mtu mwenyewe.UPO?
Delete