Vijana ni Wakati wa Kuwa Original

Inasemkana kwamba, “ni bora kushindwa katika kuwa Original kuliko kufanikiwa kwa kuiga.” Kwa bidhaa ya kondomu halisi na kongwe za kitanzania, Salama kondomu imeibuka na msemo wa “Kuwa Original” kwa ajili ya vijana. Kuwahamasisha kukubaliana na kusherehekea uhalisia wao!


Sasa, unaweza kusema “ni rahisi kutamka kuliko kutenda” ukizingatia jinsi vijana walivyo leo hii katika jamii. Kila mtu anataka kuwa mtu fulani na kila mmoja anataka mafanikio. Lakini siku zote kuna matumaini kwa wale ambao wanajitahidi/wanaopambana kuwa wajasiri na tofauti. Na kwa hilo akilini, Salama kondomu wamechukua hatua ya kuwatafuta vijana wajasiri na Original watakaosimulia hadithi zao.

Kuna wasanii wengi vijana siku hizi. Wengine hupenda kushuka mistari vyumbani mwao, baadhi katika studio gizani chini kwa chini Ubungo, bila kitu chochote bali midundo. Pia kuna baadhi yao wanapendelea kuwa katika mkumbo wa wapenzi na marafiki kuwasikiliza wakishuka misatari kama Faraji Junior, kijana wa Kitanzania akiwa ni rapa na mtunzi ambaye ni sehemu ya kundi hilo.


Pengine umeona baadhi ya hawa vijana wakiteleza na viatu vyenye matairi karibu na stendi ya mabasi ya Morocco BRT, wakifanya makeke na kuruka kwa kila mtindo. Miongoni mwao, jina lake ni Walter Mzengi, ambaye ametokea kuwa mwanzilishi na “skateboarder” wa “Tanzania Skate Society. Uhalisi wa kijana huyu Mtanzania umechochewa na ujuzi wake.

Skater 2

Umewahi kukutana na kijana mwandishi na shupavu akiwa umri wa miaka 22?! Basi kukutana na Zuhura ambaye ni kijana mshairi wa Kitanzania, mwenye kipaji cha hadithi simulizi na kueleza hisia zake kupitia sanaa ya mashairi na kunena maneno. Maneno yake yanaweza kukupa hisia kali na pia yakakupa uwazi na furaha.

Umewahi kuona kitu kawaida kilichotengenezwa kisanaa na ubunifu wa hali ya juu? Kukutana na Yvette Nkhoma, kijana wa Kitanzania mwenye kipaji cha kutengeneza urembo akitumia malighafi za kawaida. Kipaji chake kinaendeshwa na imani yake kwamba kila mwanamke ana uzuri katika dosari yake.


Umewahi kusikia ya sanaa ya ngoma ya kisasa? Kukutana na Alawi kijana wa Kitanzania ambaye ni dansa wa ngoma za kisasa mwenye uwezo wa kukonga nyoyo za umati kwa umahiri wa kipekee. Juhudi za kijana huyu zinaweza kufanana na zile za Michael Jackson katika Billie Jean na ujasiri kama Duma.



Chukua ujumbe huu; kuchukua nafasi, ishi maisha kwa uhuru lakini yenye afya, na daima kubaliana na uhalisi wako kuwa ndio njia ya furaha na mafanikio. Dumisha kaulimbiu, #KuwaOriginal #ChaguaOriginal

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad