Waisraeli huenda wanasaidia FBI kufungua simu ya Iphone ya Gaidi


Kampuni moja inayohusika katika masuala ya ya usalama mtandaoni kutoka Israel inakabilwia na shinikizo la kuitaka ieleze iwapo inasaidia idara ya uchunguzi wa jinai ya Marekani kufungua simu ya iPhone.

Idara ya FBI ilisema Jumatatu kwamba huenda imefanikiwa kupata njia ya kufungua simu ya muuaji Syed Rizwan Farook aliyewapiga risasi watu katika eneo la San Bernardino, California, mwezi Desemba.

Gazeti moja nchini Israel limeripoti kuwa wataaamu kutoka kwa kampuni hiyo ya Cellebrite wanahusika katika kesi hiyo.

Maafisa wa Cellebrite wameambia BBC kwamba huwa wanafanya kazi na FBI lakini hawakueleza zaidi.

Tovuti ya kampuni hiyo hata hivyo inasema miongoni mwa mengine kampuni hiyo ina uwezo wa kufungua na kupata habari kutoka kwa simu aina ya iPhone 5C, muundo ambao ni sawa na wa simu hiyo ya Farook.

Kampuni ya Apple, inayotengeneza simu za iPhone, imekataa kuwasaidia FBI kuifungua.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad