Wamechanganyikiwa...DALILI Zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kuukosa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam

DALILI zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuukosa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam zimedhihiri na sasa wamechanganyikiwa, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa kutoka Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam zinaeleza kwamba, CCM inaelekea kushindwa kupiga ‘bao la mkono’ kwenye uchaguzi wa Meya wa Jiji hilo kutokana na mazingira kukaa vibaya.
Leo Juma Gaddafi, Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam amekutana na baadhi ya waandishi katika Ofisi ya CCM Mkoa huo huku akionesha hofu ya chama hicho kushindwa kutetea nafasi hiyo.

Taarifa kutoka kwenye kikao hicho zinaeleza kwamba, CCM mpaka sasa imekata tamaa ya umeya kutokana na mazingira magumu yaliyotengenezwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Si hivyo tu, katibu huyo ameonesha kuchukizwa na kile alichokieleza udhaifu wa Isaya Mngurumi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala na Mkurugenzi wa Manspaa ya Kinondoni kwa kushindwa kuhimili wajumbe wa Ukawa kwenye chaguzi za umeya wa wilaya hizo.

“Wakurugenzi hawakuwa majasiri katika kupamba na vitisho vya wajumbe wa Ukawa na kuwa wakweli. Walishindwa kutoa tafsiri sahihi ya wajumbe halali wanaotakiwa kupiga kura katika uchaguzi wa meya wa jiji,” amelalamika Gadafi.

Kwenye mkutano huo Gadafi amedai kwamba wakurugenzi hao walifanya upotoshaji wa tafsiri sahihi kuhusu uwepo wa wajumbe wa CCM walioonekana kutokuwa wajumbe halali.
“CCM imesikitishwa na upotoshaji uliofanywa na wakurugenzi hao hasa kwa kuwavua uhalali wa kupiga kura baadhi ya wajumbe wetu,” amesemea na kuongeza;

“Wakurugenzi wa Manispaa za Ilala na Kinondoni wamekula matapishi yao, haiwezekani uchaguzi wa awali wawakubali wabunge viti maalum kama wajumbe halafu uchaguzi wa jiji waseme hawastahili kupiga kura.”

Gaddafi amedai kwamba, Ukawa ndio walikuwa wa kwanza kuuvuruga uchaguzi huo kwa kuwa walitumia njia ya vitisho na kuwafanya wakurugenzi wafanye maamuzi kulingana na mashinikizo yao.

Amedai kwamba, licha ya CCM kuonekana kuwa chanzo cha kuvuruga uchaguzi huo lakini chama hicho hakina sababu hata moja ya kufanya hivyo isipokuwa ni utaratibu wanaoshinikiza ufuatwe na kuwa wana mgombea bora na anayekubalika.

“Wajumbe wa Ukawa ndiyo walianza kukiuka taratibu za upigaji kura kwa kupiga picha kura walizopiga na kumuonesha mmoja kati ya viongozi wao.

“Uchaguzi hupigwa kwa siri, iweje Ukawa wawalazimishe wajumbe wao kupiga picha kura walizopiga? Ina maana wanaogopa wajumbe wao wasije wakaipigia kura CCM,”amesema.
Jumla ya wajumbe wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji ni 161. Kwa upande wa Kinondoni kuna wajumbe 58 ambapo CCM wapo 20 na ukawa 38.

Temeke jumla ya wajumbe 49, CCM wapo 31 na ukawa 18 na Ilala jumla ya wajumbe 54 huku CCM wakiwa 23 ukawa 31.

Chanzo: Mwanahalisionline
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad