Zanzibar: Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said Akamatwa na Haijulikani Alipo......Hapa Kuna Mahojiano Akiwa Kusikojulikana

Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said jana alikamatwa na watu wasiojulikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Unguja, alipokuwa akisafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia afya yake.

Akizungumzia tukio hilo jana, mume wa Salma, Ali Salim Khamis ambaye pia ni Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), alisema alipata ujumbe wa maandishi kutoka kwa mkewe kwamba amekamatwa.

Khamis alisema alipokwenda uwanja wa ndege aliambiwa na mkuu wa polisi wa uwanjani hapo kwamba hana taarifa za tukio hilo jibu ambalo alilipata pia kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi.

Alisema aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambako pia aliambiwa hawana taarifa za kukamatwa kwa Salma. “Hadi sasa sijui mke wangu yuko wapi bado naendelea kumtafuta.”

Khamis alisema Salma alikuwa tayari amepitia taratibu zote na alikuwa akisubiri kuingia ndani ya ndege ambayo haikutajwa, lakini alisema ndege hiyo iliyokuwa iondoke saa 8.05 mchana ilizuiwa na watu hao wanaodaiwa kuwa ni askari hadi saa tisa kasoro, walipoiruhusu lakini ikidaiwa kuwa waliondoka na Salma kwenda kusikojulikana.

==> Hapo chini kuna  Mahojiano ya DW na Salma Said akiwa sehemu ambayo haijulikani

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmh,lakini kama ni polisi kwa nini waogope mpaka wajifunike sura?
    Kama swala ni kuripoti mbona bado ana simu,hapo si anaendelea kuripoti?Isije kukawa kuna mchezo unachezwa,Mungu wetu simama na hawa ndugu zetu wa-Zanzibar.

    ReplyDelete
  2. Very strange. Ina maana polisi hawawezi kui trace location ya simu ya huyu mama??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad