Zari wa Diamond Adaiwa Kumpa Makavu Laivu Kajala


Kufuatia madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekuwa na katabia ka’ kujiweka kimahaba kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa Sauzi, madai yametua mezani mwa gazeti hili kuwa, kimenuka kati ya Zari na Kajala.

Chanzo chetu makini ambacho kimeomba jina lake lisitajwe gazetini kimedai kuwa, hivi karibuni baada ya Zari kupata ubuyu huo wa kuchovyewa penzi lake, alitafuta simu ya Kajala kisha kumpigia na kumpa makavu kuwa, asimuingilie kwenye himaya yake.

“Siku moja nilikuwa na Kajala, mara ikaingia simu ambapo alipopokea akasikia sauti ya Zari, basi unaambiwa akamsema sana juu ya kuingilia penzi lake, Kajala akawa kimyaa, wala hajajibu lolote, inavyoonekana alipewa makavu,” alidai mtoa habari huyo.


Baada ya kupata habari hiyo, paparazi wetu alimtafuta Kajala ili kuzungumzia madai hayo ambapo alipokea simu na kupewa mkanda mzima, alishangaa na kuuliza: “Nyie nani kawaletea hizo habari, jamani watu wambeya sana.” Alipobanwa zaidi akasema hawezi kuongelea hayo mambo.
Zari hakuweza kupatikana mara moja ila Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kupitia simu yake ambapo mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:

Ijumaa: Ebwana kuna habari kuwa Zari alimpiga mkwara Kajala juu ya tuhuma za kutoka na wewe kimapenzi sijui hilo likoje kwa upande wako?

Diamond: Hahahaa, sema nini mwanangu, hapa sikusikii vizuri nipo njiani naelekea Sweden.
Ijumaa: We nijibu tu, imekuwaje?
Diamond: Dah! Kweli mimi hata nakosa hata la kusema hapo maana mambo ya wanawake ni ngumu kuyaingilia kwa namna yoyote ile ila sijui nini hapo.
Ijumaa: Oke poa.
Kipindi cha nyuma ilidaiwa kuwa, Kajala alikuwa na uhusiano wa siri na Diamond mpaka ikafikia hatua baadhi ya watu kuhisi hata ile mimba aliyokuwa nayo Kajala ilikuwa ya msanii huyo anayefanya poa kwa sasa kwenye muziki.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnatungaga wenyewe tumewashtukia long time

    ReplyDelete
  2. du inaonekana Kajala anapenda kupitia pale Wema alipopita, mara CK sasa Diamond kwani Kajala huwezi kutafuta bwana wako mwenyewe, bibie Wema alikusaidia kukutoa jela leo hii unamuona hafai mpaka unamchukulia mabwana zake wa zamani ama kweli wanawake wa kibongo hamfai mnaweka tamaa ya pesa mbele kuliko urafiki na ndiyo maana Wema hatoweza kukusamehe kamwe hapo namuelewa Wema vizuri sana, na wewe Kajala karma is a bitch siku moja utakuja juta.

    ReplyDelete
  3. kwani huyu bibi anafikiria Domo anamkaza yeye tuu? kaingia choo cha xxxx

    ReplyDelete
  4. ATAZAA MPAKA UTUMBO. LAKINI DAI ANATEMBEA NA KAJALA NA HAJAMUACHA.

    ReplyDelete
  5. Kajala hatosheki na midume alifikiri Zari atakuwa kama Wema safari hii kakomeshwa. kama alitiwa ndo basi tena Dai atatafute mtz mwingine.

    ReplyDelete
  6. jamani mbona bibi na shangazi wameachwa sweden? tour yao vepeeee au pesa zimeisha za kiki.

    ReplyDelete
  7. bi kizee anafikiri yuko peke yake kwa Domo? awaulize walomtangulia.

    ReplyDelete
  8. huyu bibi kwanza angemuuliza Penny jinsi alivyomvumilia Dai kwa kutembea na wanawake wengine.Penny alijitahidi sana kumvumilia Dai mwishowe alichoka, itakuwa mtu mzima alokwenda leba mpaka madactari wamemchoka? azae tuuu ila ajue cku yake itafika kama si kukaribia.

    ReplyDelete
  9. Dahhhh...eti niko safarini naeleka sweden, hz habari zingine bhana, ss huko sweden anaenda na basi hadi simu yake ya mkononi ipatikane au....mnazinguaaaaa

    ReplyDelete
  10. Zari kamzalia Dai kafikiri kapata hajui kuna wengine zaidi yake. pole zake

    ReplyDelete
  11. Walaumu na CK na Dai. Si Kajala peke yake. Isitoshe CK atabaki kuwa mume wa mtu na wote tunajua hata Wema alikuwa mwizi. Hela za kumtoa Kajala zilikuwa za CK. Hata mkewe CK hatamsamehe Wema for what she had done to the family.. Idriss pia ni wa Samantha mbona Wema kampopoa ? Lets be fair.....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad