Zitto Kabwe: Tanzania Kunyimwa Fedha ni Matokeo ya Ubabe wa CCM

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema MCC kuinyima fedha Tanzania ni kwa sababu ya ubabe wa CCM na kwamba, sasa watu wasivikwe koti la uzalendo kwa jambo hilo.


Kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Zitto aliandika kuwa: “Uzalendo ni kutaka haki ya kidemokrasia Zanzibar. Haki ya Wananchi waliochagua viongozi wao Oktoba 25, 2015. 


“Sitakubali kuvishwa koti la uzalendo kwenye suala la MCC. Hilo ni suala la CCM, kukosa misaada ya Marekani ni matokeo ya ubabe wa CCM kuhusu Zanzibar.


“Haina mahusiano yeyote na uhuru wa nchi yangu. Nawasihi Wazanzibari wawe na subra Mola kamwe hatawatupa. Haki itapatikana tu. Nawasihi Watanzania kuelewa kwamba CCM ndio imetufikisha hapa na iubebe mzigo huu bila kuufanya ni mzigo wa nchi.”


Aliandika pia kwamba: “Zanzibar inatazamwa kama Zanzibar, kwa wenye maono mafupi. Nilipata kuwaambia viongozi wenzangu kwamba tishio kubwa zaidi la kutoshughulikia mtanziko wa Zanzibar ni upotoshaji. 


“Tutajikuta tunaacha kushughulika na masuala ya maendeleo kwa kipindi kirefu kidogo. Tabia ya kitanzania ya kupenda ‘shortcuts’ (njia za mkato) itatugharimu sana. You can’t just ignore Zanzibar and move on. You just can’t (huwezi ukaipuuzia Zanzibar na ukaendelea tu, huwezi).” 


Pia Mbunge huyo aliandika kuwa: “Serikali ya Marekani imesitisha mahusiano na Serikali ya Tanzania kwenye miradi ya MCC. 

“Hivyo Tanzania itakosa Sh. trilioni moja ambazo zilikuwa zimeelekezwa kwenye umeme na umeme vijijini. 

“Sababu? Zanzibar na Cybercrime Act. Siku si nyingi tutawasikia Umoja wa Ulaya nao. Nasubiri kusikia Serikali ya Rais Magufuli itasema nini. 


“Suala la Zanzibar likitazamwa kibabe kwa kuwa watawala wana maguvu nchi itaingia kwenye matatizo makubwa sana ya ndani bila kujali misaada inakatwa au la. Sipendi misaada. Sipendi mataifa ya kigeni kuingilia masuala yetu ya ndani. 


“Lakini Tanzania sio kisiwa, tunaishi ndani ya jamii ya kimataifa. Kuna mambo lazima tufanye kwa kuzingatia misingi ya kidunia. Zanzibar ni moja ya jambo hilo. Tusiweke kichwa kwenye mchanga kama mbuni.”


Naye Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje wa Chama Cha ACT-Wazalendp, Theopister Kumwenda, alisema uamuzi huo wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini. 


Alisema ACT-Wazlendo inatambua kuwa katika kipindi hiki Tanzania inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwamo MCC, katika kuendeleza miradi  ya maendeleo. 


Alisema MCC imekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijijini

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi hawa viongozi wa upinzani wako timamu kweli?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanaweweseka bado na dawa ni kuachana nao,umiza kichwa na kuvuja jasho kwa ajili ya mwananchi sio mpinzani.

      Delete
    2. HUJUI UNACHOKIANDIKA KWA SIASA ZA KISHABIKI WATANZANIA TUNAUMIA KWA AJIRI YA CCM....THEN KWA KUWA UNA SHART NA KOFIA UNAONA MCC JAMBO DOGO

      Delete
  2. MH Zito mpaka sasa Zanzibar suala la Umeme halina tatizo kuanzia mjini hadi vijiji umeme upo wamerekani wakinuna wezao wapo wanaotaka kuunda udugu wa kibiashara kwa mfano Japani na China

    ReplyDelete
  3. Zito mpuuzi, Egpty au Misri ni nchi ya pili inayopokea misaada mikubwa ya Marekani baada ya Israili licha ya serikali ya kidikteta wa jeshi wa Misri kuipundua serikali halali ya raisi Mohammed Morsi. Sasa hapa wanasiasa hawaoni kama wamarekani wanatupiga changa la macho na kutunyanyasa na misaada yao kwa kisingizio cha demokrasi? Kiongozi yeyote wa nchi au chama cha siasa anaekaa na kufikiria misaada ndio msingi wa maendeleo basi inabidi tathmini.

    ReplyDelete
  4. HAHAHAHAHA!AFRICA NI LAZIMA MTAWALIWE@DONALD TRUMPH.
    BILA MISAADA HAMUWEZI KUISHI?

    ReplyDelete
  5. Kwa hiyo ni mazoea vizazi na vizazi
    kutegemea misaada?hakuna mwisho?lini tutaanza kusaidia wenzetu walio maskini zaidi yetu?

    ReplyDelete
  6. wako timamu sana tu

    ReplyDelete
  7. UNAANZA UKUNGU NA WEWE?UBABE GANI WA CCM?NCHI IKO MAHALI PABAYA LAKINI TUKIUNGANA TUKAMSAIDI JPJM TUNAWEZA KUJIENDESHA BILA KUTEGEMEA WAHISANI.LEO HII KILA MCHINA ALIE VICHOCHORONI AMEKUWA MJANJA WA KUCHUMA KWA UHALIFU HATA KWA KIFICHO KUPELEKA KWAO,JE SIO HAZINA YA KUTOSHA HIYO?NA TENA JIULIZE HAO WANAOSHIKWA KILA SIKU WAMEANZA LINI,NA JE WAKO MANGAPI AMBAO HAWAKAMATWI?MBAYA ZAIDI WAPINZANI MMEKUWA WATU WA KUKATISHA TAMAA TU,KWANI NCHI NI YA NANI?

    ReplyDelete
  8. Hii nchi demokrasia bado saaanaaa,sbb hy zito kabwe ni mnafiki wa kwanza kwa zanzibar,yyndo alisema kua ule uchaguzi wa marudio si wa haki,kisha walipoitwa chemba na CCM wakaahidiwa watapewa umakamo wa kwanza wa rais wanafiki hao wakakubali na wakaeka mpk mawakala wa kusimamia kura zao,ss jamani hebu tujiulizeni hv kweli kuna chama ambacho kitatuletea haki sawa cc wananchi?kwakweli watanzania wenzangu tumuombe mola atusaidie sana,hali zetu ni mbaya japokua wengine hawataki kukubali lkn hali ni mbaya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad