Ali Kiba na Diamond Wazipige Ngumi ili Tujue Kama Kweli Wana Beef – Mzee Yussuf

Mzee Yussuf ni miongoni mwa wasanii ambao hawaamini kama Diamond na Ali Kiba wana beef kutokana na wawili hao kutokutana pamoja na kuonyesha tofauti zao.

Akizungumza  Jumamosi hii, Mzee Yussuf amesema beef ya Diamond na Ali Kiba zinakuzwa na mashabiki lakini sio beef kweli.

“Mimi Ali Kiba na Diamond sidhani kama wana beef kweli,” alisema Mzee Yussuf. “Bado siamini kwa sababu ni watu ambao hawakutani tukaona kama kweli ni beef kweli zikapigwa ngumi watu tukaona,”

Aliongeza, “Kwenye taarab kuna beef za kweli, watu wanazipiga kweli. Mimi naamini wanaume hawanuniani,”

Katika hatua nyingine Mzee Yussuf amesema anajipanga na wasanii wenzake kuanzisha umoja wa wasanii wa taarab ili na wao waweze kupeleka kero zao kwa pamoja.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Du!huo Ushauri wa Mzee Yusufu sasa umepitiliza,ngumi tena!Sikutegemea kama angeshauri hili hata kama ni utani!
    Je,Umeipata hii?Rais Magufuli jana alienda Benki ya CRDB katika branch moja jijini Dar Es salaam akiwa katika gari la private,Kuipata habari zaidi,Bofya http://goo.gl/hy20xu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad