Aliyemtukana Mtume Kuadhibiwa Kifo Nchini Mauritania

Mahakama ya Rufaa ya Mauritania imepasisha hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).

Shirika la Habari la Kimataifa la Qur'ani (IQNA) limeripoti kuwa, Mahakama ya Rufaa ya mji wa Nawadibo huko kaskazini magharibi mwa Mauritania imepasisha hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi Muhammad Sheikh Ould Amkhtir wa nchi hiyo kwa sababu ya kuandika makala iliyomvunjia heshima na kumtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw) hapo mwaka 2014.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mauritania ambaye aliomba kutolewe hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo amesema kuwa kunyongwa kwake kutakuwa somo kwa wale wote wanaothubutu kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Kuchapishwa kwa makala ya mandishi Muhammad Sheikh Ould Amkhtir hapo mwaka 2014 kulisababisha maandamano makubwa kote Mauritania ambayo hayakutulia ila baada ya kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. duniani kuna dini nyingi sisi ya kwetu inatufundisha samehe 7 mara 70.

    ReplyDelete
  2. pumba juu ya pumba

    ReplyDelete
  3. Binadamu ni wa ajabu sana. Unataka kuua binadamu mwenzio kisa kamsema vibaya mtu ambaye wala hatukuwahi kumuona zaidi ya kusikia tu habari zake. Tujiulize je angekuja huyo Mtume hapa kweli angeruhusu huyu ndugu kuuawa????

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad