Askofu Josephat Gwajima Apinga kauli ya mkuu wa Mkoa wa Arusha ya Kutaka kuyadhibiti Makanisa ya kilokole katika Makazi ya watu.

April 5 mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Arusha mh. Daud Felix Ntibenda alitoa amri ya kuyadhibiti makanisa ya kilokole jijini Arusha kwa madai kuwa yanawasumbua wananchi kwa kupiga vinanda na kuimba usiku kucha.

Ntibenda alitoa  amri  hiyo  ofisini kwake   wakati akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa yote ya jiji la Arusha.

Alisema hataweza kuvumilia makanisa hayo kuzinduliwa kila mahali katika makazi ya watu na kufanya ibada usiku kucha.

"Mimi ni mkristo, sikatazi waumini kusali, lakini nataka kuwe na utaratibu maalumu, sio kila kukicha unakuta kanisa jipya na kibaya zaidi yanasumbua hata wageni wanaoingia jijini hapa." Alisema Ntibenda.

Kutokana na kauli hiyo ya mkuu wa mkoa, Askofu Mkuu wa Kanisa na Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima  amejitokeza hadharani kupinga kauli hiyo.

Gwajima amesema Tanzania ni nchi huru, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, kila mtu ana haki ya kuabudu muda wowote na wakati wowote atakao bila kuingiliwa na mtu yeyote.

Amesema waumini wa makanisa ya kilokole Tanzania wako zaidi ya milioni 11, hivyo kuwazuia kuabudu ni sawa na kutafuta matatizo mengine

Gwajima  amesema waumini wa Kiislam huamka saa kumi usiku kuswali kwa sauti kubwa na hakuna mtu huwaingilia kwa kuwa hiyo ni haki yao kikatiba.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naona jambo moja kubwa kwa mtumishi Gwajima_hajui mipaka ya uhuru wa kuabudu. Huwezi kuabudu usiku kucha ukipiga kelele na kusumbua wasio husika na mahubiri yako.

    Hata Biblia inasema mungu wetu ni mungu wa utaratibu....... Pia inasisitiza kusali kwa hekima.... Tusiwe kama wale wanafiki wanopayuka payuka ili waonekane. Someni vizuri biblia enyi mnaojiita walokole.

    ReplyDelete
  2. kweli kabisa Mungu wetu si Mungu wa makelele... kwanza gwajima ana ulokole gani?? atuambie na uaskofu wake aliupataje? akwende zake huko....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad