Baada ya Anne Kilango Kufutwa Kazi Rais Magufuli Awashukia Mawaziri na Makatibu Wakuu..Adai Wakishindwa Waache Kazi

Dakika chache baada ya kutangaza kumuondoa Anne Kilango Malecela katika nafasi ya Ukuu wa Mkoa wa Shinyanga siku 22 tu baada ya kumuapisha, Rais John Magufuli ametoa onyo kwa Mawaziri na Makatibu wakuu aliowateua.

Akizungumza leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ameeleza kuwa anafahamu wapo baadhi ya mawaziri na Makatibu wakuu ambao wamekuwa wakilalamika ‘chinichini’ kuhusu upatikanaji mdogo wa fedha zinazoelekezwa katika matumizi mengine, yaani OC (Other Charges).

Amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kuwaonya Makatibu Wakuu wanaoanza kulalamika na kudai waongezewe OC na kwamba kama kuna anayeona fedha zinazotengwa ni chache ajiondoe.

“Chief Secretary, huo ndio muelekeo kwa Makatibu Wakuu wengine, waache kudai OC… ninawasikia. Wapo wanaodai OC ni chache, wakiona ni chache waache kazi. Wenzao wabunge wanasema ni nyingi,” alisema.

Rais Magufuli amesema kuwa ametuma watu waweze kuwarekodi mawaziri ambao wanalalamika ‘chinichini’ kuhusu OC akieleza kuwa watu hao bado wanadhani wako kwenye mfumo uliopita.

“Kuna mpaka Mawaziri wengine naona wanalalamika, nawatafutatafuta… nimetuma watu wawarekodi kwa sababu mind set yao bado haijabadilika. Wanafikiri bado tuko kwenye treni hiyohiyo. They will go,” Rasi Magufuli alisema kwa msisitizo.

Awali, Rais Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela kutokana na kutoa taarifa kuwa hakuna mfanyakazi hewa kwenye Mkoa wake wakati timu ya Ikulu ilibainia uwepo wa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza ya ukaguzi.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahahhahah baba kanyaga twendeee pumbavuuuuu kabisaaa wanadhani wapo kwenye treni ile ile hahahhaha napenda kufanya kazi na mtu wa aina hii safi sana....kanyaga baba kanyaga wese mpka abiria waombe poo hahahhahahahahahha

    ReplyDelete
  2. Safi uncle magu.. vzuri sana tunapenda kazi yako

    ReplyDelete
  3. They have to go...........

    ReplyDelete
  4. Yes they have to go. tena wasipate hata muda wa kujieleza hawa na uncle magu usipoteze muda kuwasikiliza. chapa kazi tupate Elimu bora na viwanda. Tena usipoteze muda kuangalia sheria zinasemaje na kaa mbali kabisa na hao washauri wako watakupotosha tu.

    ReplyDelete
  5. She..nz walizoea kujilimbikizia na marushwa na wizi juu. Sasa mwisho. Kanyaga treni baba. Tena sio ile treni ya zamani rocomotive hapana electricle tren inayokwenda na wakati digital zaidi sio analog. Mungu akulinde na kukubariki. Muda wa kunyeyekea viongozi wazembe ushapitwa na wakati. Hamna mtawala mkoloni, mkoloni alisha jiondokea muda hana hata habalii. Sasa kwa nini kuwe na mabwana na watwana hpaa ni kazi tu kiongozi aliechaguliwa na wanachi na viongozi waliochaguliwa na raisi kusimamia maslahi ya nchi. Sio kusimamia maslahi yao.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad