Vitendo vya kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu limeendelea kushamiri kwenye maeneo mengi nchini tukio la sasa likitokea katika kijiji cha njani wilayani Arumeru ambapo mtoto wa kike mweye ulemavu wa viungo amebainika kufungiwa ndani kwa kipindi cha umri wake wote wa miaka kumi na sita.
Mtoto huyo Wine Ruth anayelelewa na bibi yake baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi mara baada tu ya kugundua kuwa ana ulemavu amegundulika wakati wa zoezi la kuwaorodhesha watoto wenye ulemavu wilayani Arumeru ambapo bibi yake Veraelly Ndetaulo anakiri kumfungia kwa ajili ya usalama wake anapokwenda kuwatafutia rizi wajukuu zake.
Akizungumzia tukio hilo Mbunge wa Viti Maalum Walemavu Dk.Elly Macha aliyeongoza zoezi la kumtoa ndani mtoto huyo anasema imefika wakati sasa jamii ikatambua kuwa malezi ya watoto wa kundi hilo ni la kushirikishana hasa ikizingatiwa kuwa wengi wamekua wakitokea kwenye familia zenye kipato duni.
Maisha ya Bibi Ndetaulo anayemlea mtoto huyo mwenye ulemavu,pamoja na mdogo wake ni magumu kulingana na umri wake,wadau walioshiriki kwenye zoezi la kumtoa mtoto huyo likiwemo Jeshi la Polisi wilayani Arumeru wanashauri kuwa ipo haja kwa Serikali ya kijiji kuangalia uwezekano wa kumsaidia.
Binti Mwenye Ulemavu Afungiwa Ndani Kwa Miaka Kumi na Sita Arumeru
0
April 07, 2016
Tags