Breaking News: Rais wa Zanzibar Dr Shein atangaza rasmi kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa


Akihutubia katika uzinduzi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM. 

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa isipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa mantiki hii naiona hali ya hatari ikikaribia zanzibar, lengo la serikali ya umoja lilikua kuondoa hatari iliyopo kutokana na siasa za zanzibar, lakini haya yaliyotokea ni wazi kwamba zanzibar itarudi katika hali ile ya mwanzo, na sidhani kama kuna anaependezwa na hali hiyo. Na siamini kwamba wazanzibari wameukataa upinzani ila yaliyotokea ndio yaliyoleta mgongano na kufikia hali iliyopo sasa.Kuwaaminisha wazanzibar kwamba hawautaki upinzani ispokua ccm tu, hii nayo itakua ni ishu nyingine itakayo palilia chuki na uhasama zaidi. Hivyo basi vizuri busara ingetumika zaidi bila kujali itikadi za vyama ili kuleta matumaini ya amani na usalama kwa zanzibar.

    ReplyDelete
  2. Dikteta Katika ubora wake

    ReplyDelete
  3. Ndo mlokuwa mnalitaka ilo wahuni wakubwa ccm.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad