Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mama Anna kilango Malecelakuanzia leo.
Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa sana na hali hiyo.
Amesema idadi ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili za mkoa huo bado zinaendelea kuhakikiwa.
Rais pia ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachikwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi akiwa amedumu katika nafasi hiyo kwa mwezi mmoja tu..
POLE MAMA!!!
ReplyDeleteHatufanyi kazi kwa mazoea, JPM wanyooshe Tu, hdi tutaheshimu kuwa cheo Ni dhamana na sio amana
ReplyDeleteHahaha wacha idadi ya majipu iendelee huu ni utawala wa kutumbua majipu. well done jpm
ReplyDeletesaaafi saaana Mhs Magufuli, ussiwaachie hawa, piga chini tu, wamezoea kufanya kazi kimazoea na kubebwabebwa, hii siyo AWAMU YA NNE bana, kuoneana huruma huku wananchi wakilia, HAPA KAZI TU!
ReplyDeleteHapa Kazi tu
ReplyDeleteHapa tutapata kigugumizi. Mwaya Anna pumzika na mzee wako mle pension isiwe taabu.
ReplyDeleteHahahhahahahahhahahahahahah ccm ni ile oooh ni ileee....shinyanga mnasemajeeee hahahah tumejipanga mwaka huu wataisoma wataisoma namba
ReplyDeleteHilo jipu mama. Wazembe, wavivu, wala rushwa, wakwepa kodi muda wenu umeisha sasa mtabaki kuisoma namba tu. Hapa kazi tu
ReplyDeleteHilo jipu mama. Wazembe, wavivu, wala rushwa, wakwepa kodi muda wenu umeisha sasa mtabaki kuisoma namba tu. Hapa kazi tu
ReplyDeletepole sana mwanamke shujaa wa tanzania kwa kupoteza kazi... dah kwa ile kweli nimejisikia vibaya sana kwa hatua aliyochukua huyo mh. ni zaidi ya kukurupuka.,. ameshindwa kukuonya hata onyo la kwanza! utadhani na wewe jipu wa makontena! jamani!! Mungu akutie nguvu naamini wewe ni mwanamke shujaa utasimama!JPM??????
ReplyDeletefala wew
Deleteinaonyesha jinsi gani ulivyo kilaza
majizi unayaita shuja
DeleteHili kwa Anna sio jipu ni chunusi. Labda jipu kwa afisa aliyetoa taarifa ya uongo. Ripoti ya uchunguzi angepatiwa RC. Halafu yeye ndio angemfukuza kazi huyo Afisa Tawala.JPM hapa kachemsha. Mwanamke wa shoka kama huyo angepewa onyo tu na kwamba awe makini na watendaji wake lakini dio kumwachisha. Imeniboa.
ReplyDeleteMwanamke shujaa wa kuficha majipu sugu? Acheni kuwadhililisha akina mama zetu kwa kuwapa ushujaa wa hovyo,they are far better than that.
ReplyDeleteHujamsikiliza hoja zake bungeni?
ReplyDeletehoja za bungeni na ukuu wa mkoa ni tofauti sana, jamani alipokuwa anaapishwa si mwajili wao aliwaambia wakafanye kazi gani kwanza???? alitakiwa ajiridhishe kwanza kabla ya kutangaza kwenye press, hapa tatizo ni kufanya kazi kwa mazoea, tuache hizo bhana
Deletepole mama anne hayo ni mapito tu! kwani hata yeye mtumbua majipu ni binadamu ana madhaifu yake je yeye ni nani atakaye mtumbua jipu?
ReplyDelete