Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Bulembo amemtaka waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amwache Rais Magufuli aendelee kufanya kazi zake.
Bulembo anakuwa kiongozi wa pili wa CCM kumvaa Lowassa aliyekosoa utendaji wa Rais Magufuli wa kutumbua majipu wakati alipokutana na wanazuoni wa ndani na nje ya nje Alhamisi ya wiki hii, baada ya juzi msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka naye kumkosoa kuwa si kweli kwamba watumishi wa umma wanafukuzwa bila kusikilizwa.
Akizungumza mjini hapa jana na wanachama wenzake wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Jumuiya hiyo yaliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro, Bulembo alimtaka Lowassa kutekeleza ahadi yake ya kwenda Monduli kuchunga ng'ombe kama hatochaguliwa kuwa Rais.
"Kama yeye anasema kasi ya Magufuli ni ya muda au anakosea kutumbua majipu, basi tunamkumbusha kauli yake wakati akiongea na vyombo vya habari kuwa akishindwa urais atarudi kijijini kwake kuchunga ng'ombe, tunaomba aende akafanye kazi aliyoahidi. " Alisema Bulembo.
Alisema anashangazwa na Liwassa aliyekuwa mgombea urais mwaka jana kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa UKAWA kusema ndani ya CCM kumejaa ufisadi wakati yeye ni fisadi namba moja.
Katika hatua nyingine, Bulembo alisema ndani ya CCM kuna majipu yanayohitaji kutumbuliwa wakiwemo Wasaliti.
Alisema wanasubiri Rais Magufuli akabidhiwe uenyekiti wa CCM mwezi wa saba mwaka huu ili waanze kuyatumbua majipu hayo.
Bulembo: Lowassa ni Fisadi, Namshauri Amwache Rais Magufuli na Badala yake Aende Kijijini Kuchunga Ng'ombe
2
April 10, 2016
Tags
Hii dhana yakutumbua majipu siilewi vizuri, maana hii nchi tokea kukabidhiwa na mkoloni serikali imeongozwa na CCM mpaka leo, na hayo majipu yote yameletwa na CCM na wanaCCM, sasa anapotokea mwanaCCM leo hii nakusema anatumbua majipu nakua simuelewi. Hivi kweli jipu laweza kujitumbua lenyewe?
ReplyDeletewe bora ukae kimya, maana hata kwenye familia yako wapo ambao hamwendani nao kila mtu ana hulka yake, ndani ya ccm kila mtu ana hulka yake wapo wasafi na waroho kwa hiyo Rais aliyepo sasa siyo kama huyo aliyepita kwa sababu kipindi kile hakuwa na meno ya kung'ata na ndo maana alisema atatumbua majipu na hilo siyo kwa ccm peke yake hilo litamgusa kila mtu aliyejilimbikizia mali kwa kutomwogopa Mwenyezi mungu wakati kuna kundi kubwa la walala hoi wanaoteseke. tumwache Rais afanye kazi ili tunyooke
Delete