Kati ya vyama 22 vya siasa vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja tukilichopeleka hesabu zake kukaguliwa kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzoni mwaka 2015.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, alikitaja chama hicho kuwa ni Chama cha Wananchi (CUF), kilichopeleka hesabu zake za kuanzia Januari mpaka Juni 2015, huku vyama vingine 21 vikishindwa kufanya hivyo, kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 14 cha sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992.
“...na hili lifahamike kuwa, siyo katika kipindi hicho, hata leo (jana) nimeuliza wasaidizi wangu kama wameshaleta au bado lakini naambiwa ni chama kimoja,” alisema.
Alipendekeza ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kufuatilia suala hilo ili uwasilishaji wa taarifa za fedha ufanywe kwa wakati kulingana na matakwa ya kisheria.