CCM ni ile ile -Zitto Kabwe

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema Chama Cha Mapinduzi CCM ni kile kile cha siku zote, Zitto Kabwe amesema hayo baada ya kusoma vitabu vya Bajeti ya mwaka huu na kusema kuwa bajeti hiyo ni ya kulipa deni la Taifa.

Kwa Mujibu wa Zitto Kabwe amedai kuwa Serikali inatarajia kukusanya shilingi trilion 17 kwa mwaka na kusema zaidi ya tirioni 8 zitakwenda kulipa deni la Taifa ambalo ni zaidi ya asilimia 50 ya bajeti na kusema ukichanganya na mishahara ya watumishi ambayo huwa ni nusu ya bajeti ni dhahiri kwamba makusanyo ya Serikali yataishia kulipa madeni na wafanyakazi.

"Nimemaliza kusoma vitabu vya Bajeti ya mwaka huu. Kimsingi ni Bajeti ya kulipa Deni la Taifa.

Wakati Serikali inatarajia kukusanya shilingi trilion 17 mwaka huu, shiling trilioni 8 ikiwa ni asilimia 50 italipia Deni la Taifa. Ukiweka na mishahara ya watumishi ambayo huwa ni nusu ya bajeti, ina maana makusanyo yote ya Serikali yatalipia madeni na mishahara.

Ndiyo maana Serikali inaenda kukopa zaidi ya shilingi trilion 7 mwaka huu na kutegemea misaada ya wafadhili kwa shilingi trilion 5. CCM ni ile ile, ile ile....." aliandika Zitto Kabwe

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. zito mbona unavuka mpaka kwani wewe ni nani hebu jiulize kwanini Iwe wewe ndio msemaji unchukiza ccm ni ile ile ndio ilio kulea hebu tulia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli Kabisa bahati Yao CCM wanamtumia magufuli tuuu
      Magufuli Upo chama kibovu
      Ungekuwa UKAWA kweli tungeona mafanikio ya kweli kwa Watanzania

      Delete
  2. Hizi ndio zake..SIASA NA SKENDO ...TUNATAKA MAENDELEO YA NCHI..HUNA YNAKAA BENCHI KUMBUKA KUTIA SAINI MAHUSHURIO NA LAIVU HAKUNA..BWETEKA HIKI KIPINDI.. UKIMALIZA TUNARUDIA UANDIKISHAJI WA VYAMA UPYA .NA SERA ZA MAENDWLWO NA MITIHANI MITATU ..1 UZAKENDO. 2. ELIMI. 3, UKIPEWA NAFASI UNAHISI UTAKETA MABADILIKO GANI YA NAENSELEO KTK BCHI (UNAANDIKA NA KUJIELEZA) HII NI BAADA YA KUKUONENI KWAMBA. KAZI NA KUWAJUBIKA KWA WAPIGA KURA ZENU. HAMUWATENDEI HAKI NA WAJIBU AMBAO WAO WANEKUPENI...UPO ZITTO..HAPA NI KAZI TU

    ReplyDelete
  3. Dogo Ni mchumi ..Dogo Ni mwanasiasa chipukizi....Dogo mwanasheria...Dogo Mpelelezi..Dogo Hakimu...Dogo Ni Rahisi Mtarajiwa...Dogo Chizi wetu dam damu...BARIDA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad