CHADEMA Yazidi Kuvunjika Mwanza..Aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Mkoa wa Mwanza Ajivua Uanachama

Aliyekuwa Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba ametangaza kujivua uanchama na kuachana na siasa.

Tizeba aliyesimamishwa uongozi na Baraza la Uongozi la Chadema tangu Mei 4, mwaka jana, alisema hatajiunga na chama chochote cha siasa.

Kwa uamuzi huo, Tizeba amepoteza nyadhifa zake zote ikiwamo ya uenyekiti wa Baraza la uongozi la mkoa na ujumbe wa Baraza la Uongozi Kanda ya Ziwa.

Mei 5, mwaka jana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, wakati huo, Dk Willibrod Slaa, alimuandikia barua Tizeba yenye Kumb Na C/HO/ADM/KK/08 ,kumsimamisha uongozi wa chama hicho.

Akizungumzia uamuzi wa kiongozi huyo kujivua uanachama na kuachana na siasa, Mratibu wa Chadema Kanda ya Ziwa, Renatus Bujiku alisema chama hicho kimepokea kwa mshtuko taarifa hizo kwa sababu bado suala lake lilikuwa linashughulikiwa.

“Utaratibu wa chama ulikuwa unaendelea kushughulikia suala lake, nadhani kachukua uamuzi wa haraka,” alisema Bujiku.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na bado,watatoka wengi tu na wengine kurudi CCM.
    Wako wanaojiita CHADEMA lakini cadi ya CCM hawajarudisha na imekuwa mwiko kwao kuvaa Sare au magwanda ya CHADEMA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Endelea kujitekenya baba ukichoka wanaume tutakuja kukutekenya,wanaume hatufuati bendera kifala hivyo,tunaangalia utendaji wa magufuli siyo utendaji wa ccm.

      Delete
    2. WALA HAJAKOSEA,KWANI MAGUFULI KATOKA UKAWA?AU
      ANATUMIA KATIBA YA UKAWA?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad