Clouds FM Yaendeleza Nyakua Nyakua ya Watangazaji na Madj..Wamewachukua Hawa East Africa Radio


Ile Vuta N’kuvute ya vituo vya redio inaendelea na sasa East Africa Radio imekuwa mhanga mpya.

Dj wa kike, Sinyorita na mtangazaji wa The Cruise, Mami wanadaiwa kuondoka East Africa Radio kuanzia wiki hii baada ya kupata dau kubwa kutoka kwa guess what? Clouds FM.

Tetesi hizo zilianza kuvuma tangu wiki iliyopita lakini jana zimeonekana kupata ukweli baada ya wawili hao kutosikika kwenye kipindi cha The Cruise, kitu ambacho si cha kawaida.

Tetesi zinadai kuwa tangu Dj Fetty aache kazi Clouds FM, wamekuwa wakitafuta mtangazaji wa kike anayeweza kuchukua nafasi yake na Mami anaonesha kuwa na caliber hiyo.

Tayari wawili hao wamebadilisha profile zao za Instagram kwa kuondoa kipengele cha kuwa ni wafanyakazi wa East Africa Radio.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad