CUF Yaitolea Uvivu China Baada ya Kudai Uchaguzi wa Marudio Zanzibar Ulikuwa Huru na Wa Haki

Siku moja baada ya Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing kusema kuwa nchi yake inaamini kuwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Zanzibar hivi karibuni ulikuwa huru na haki, chama cha CUF kimejitokeza na kupinga kauli hiyo kikieleza ni ukandamizaji wa demokrasia.

Chama hicho kimeionya China kuacha siasa na kufumbia macho ukiukwaji wa demokrasia nchini kwa masilahi yao na kuitumia Tanzania kujinufaisha na rasilimali zilizopo bila kujali amani itakapovunjika hapo baadaye.

Juzi, Dk Youqing alipokuwa anazungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba alimhakikishia kuwa nchi yake itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania hata baada ya Shirika la Marekani la Maendeleo ya Milenia (MCC) kusitisha misaada.

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Abdalah Mtolea alisema China inahalalisha uchaguzi wa marudio uliofanyika Zanzibar kwa sababu ya masilahi yao ya kiuchumi kwa taifa lao na raia wa China waliopo nchini.

“CUF tunaelewa kwamba kwa nchi yoyote inayofahamu demokrasia, uhuru na haki ni nini, hawezi kusema uchaguzi wa marudio Zanzibar ulikuwa huru na haki,” alisema.

Alisema chama kikongwe kinachotawala China CCP na CCM vimekuwa na uswahiba wa muda mrefu jambo linaloifanya nchi hiyo kutoaana mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa demokrasia na haki za binadamu wakihofia kuharibu uhusiano wao.

Alisema Serikali ya Tanzania inapaswa kuwa makini na uhusiano na misaada inayotolewa na nchi hiyo ili kubaini  ina malengo gani yaliyofichika kwa Taifa letu.

Mtolea ambaye pia ni Mbunge wa Temeke alisema China imeamua kuunga mkono kukandamizwa kwa demokrasia nchini Tanzania ili kujikomba kwa Serikali ya CCM waendelee kupata hisani zaidi kwa masilahi ya taifa lao.

Alisema: “China inapata tenda kubwa za ujenzi nchini Tanzania mfano ujenzi wa barabara ambazo nyingine zishaanza kuharibika, madaraja na majengo makubwa nchini.

"Hata mradi wa kusafirisha gesi, kana kwamba hiyo haitoshi, kumekuwa na ongezeko la Wachina wakifanya biashara zinazofanywa na Watanzania huku wengine wakiishi nchini bila vibali."

Katika mazungumzo yake na Waziri Makamba, Balozi Youqing alisema China ina mipango mingi ya ushirikiano na Tanzania, ikiwamo kwenye sekta ya umeme na itaendelea kutoa ushirikiano kupitia kampuni zake.

Kwa upande wake, Makamba alimshukuru Balozi Youqing pamoja na Serikali ya China kwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

“Ujumbe na salamu ulizotoa leo umetupa faraja Watanzania. Urafiki baina ya nchi zetu, na baina ya vyama vyetu vya CCM na CCP, ni wa muda mrefu, ni wa majira yote na umejengwa kwenye misingi ya kuheshimiana na hauna budi kuendelezwa”, alisema Makamba.

Pia Waziri Makamba na Balozi Youqing walikubaliana kutembelea Pemba na Unguja kwa pamoja ili kukagua na kutengeneza miradi ya maendeleo kati ya China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watajuta marekani china karibuni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa wamarekani watajuta kwa kitu gani?Wana jaribu kutetea demokrasi.

      Delete
  2. China ni watu wa kuogopws ssna Tanzania. Mwa vile watanzania bado wengi tumelala zchina itsmiliki njis zote kuu za uchumi wa nchi hii sababu vionhozi walioserikalini wamefanya China ksma wajomba zao. Ni uduni wafikra kujua zchina na missada michafu ndiyo insyoua uchumi na maendeleo nchini. Viongozi wadio na upeo wa kufikiri haeawezi kutenganisha kati ya undugu na ueekezaji.zmchina snamamlaka makubwa Tanzania kuliko viongozi wa tanzania. Watawaingiza wachina wengi nchini wasio na elimu watafanya vibarua ns kuiba, kufanya magendo, kutorosha mali na utajiri wa chi hii kama yao huku watanzsnis wasomi wakiwaangalia. Wanachosema Cuf ni kitu kikubwa sana na kichukuliwe maanani.wapinzani wananysnyaswa lakini wsnaona mbele kuliko watu wa ccm. Wachina wanagombea mikataba Zanzibar huenda wameshapewa dili na wakuu.Mtanzania ndiye aliwaye ssbsbu wengi hawaoni mbele. Wachina wanstoa missada hii ni hongo ya kujiingiza zaidi nchini. Mchins Tanzania. Ni mali yake kisha iweka mkononi. Ni China insyojihusisha na viongozi wetu wakuu kuinyonya Tanzania. Mchina atakufanya rafiki na staingia kijijini kula ugali nawe ili apate siri zote na atapewa bure huku mkimchekelea na atakomba kila kitu. Subirini tu. Mikstaba ya China Tanzania itakuja kulia. si sawa na na ile ya ujenzi wa reli ya zamani.mikataba ya sasa ni umiliki wa njia kuu zote za nchi hii. Malipo yake watanzania nchini watawafanyia kazi na kuwalipa wachina.mmejiletea utumwa mwingine.ukiwaona maraisi wanapokaa na maraisi wa wa China ni amri tupu lakini amri ya kiaina yake. Ni ya kitulivu sana yenye tabasamu na nyororo huku unaliwa. Hatuna akili.

    ReplyDelete
  3. China ni watu wa kuogopws ssna Tanzania. Mwa vile watanzania bado wengi tumelala zchina itsmiliki njis zote kuu za uchumi wa nchi hii sababu vionhozi walioserikalini wamefanya China ksma wajomba zao. Ni uduni wafikra kujua zchina na missada michafu ndiyo insyoua uchumi na maendeleo nchini. Viongozi wadio na upeo wa kufikiri haeawezi kutenganisha kati ya undugu na ueekezaji.zmchina snamamlaka makubwa Tanzania kuliko viongozi wa tanzania. Watawaingiza wachina wengi nchini wasio na elimu watafanya vibarua ns kuiba, kufanya magendo, kutorosha mali na utajiri wa chi hii kama yao huku watanzsnis wasomi wakiwaangalia. Wanachosema Cuf ni kitu kikubwa sana na kichukuliwe maanani.wapinzani wananysnyaswa lakini wsnaona mbele kuliko watu wa ccm. Wachina wanagombea mikataba Zanzibar huenda wameshapewa dili na wakuu.Mtanzania ndiye aliwaye ssbsbu wengi hawaoni mbele. Wachina wanstoa missada hii ni hongo ya kujiingiza zaidi nchini. Mchina Tanzania. Ni mali yake kisha iweka mkononi. Ni China insyojihusisha na viongozi wetu wakuu kuinyonya Tanzania. Mchina atakufanya rafiki na staingia kijijini kula ugali nawe ili apate siri zote na atapewa bure huku mkimchekelea na atakomba kila kitu. Subirini tu. Mikataba ya China Tanzania itakuja kulia. si sawa na na ile ya ujenzi wa reli ya zamani.mikataba ya sasa ni umiliki wa njia kuu zote za nchi hii. Malipo yake watanzania nchini watawafanyia kazi na kuwalipa wachina.mmejiletea utumwa mwingine.ukiwaona maraisi wanapokaa na maraisi wa wa China ni amri tupu lakini amri ya kiaina yake. Ni ya kitulivu sana yenye tabasamu na nyororo huku unaliwa. Hatuna akili. Bado hatujui kujiongoza wenyewe wala kufikiri.mnawanyamazisha wenye akili kwa woga wa kufichua mambo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad