Diamond Akitaka Kuandika Wimbo wa Kuumizwa Kimapenzi Humfikiria Msichana Huyu (Audio)

Diamond Platnumz ni bingwa wa kuandika nyimbo za kuachwa, kuumizwa na kutendwa kimapenzi.

Kamwambie, Mbagala, Mawazo, Ukimwona, Nataka Kulewa, Bado na zingine, zilihit kwasababu ziligusa maisha ya wanaume wengine wahanga wa malavidavi. Lakini staa huyo ambaye hivi karibuni alisema Zari ameutunza moyo wake kwenye friji kiasi cha masuala ya kuumizwa kuyasikia tu kwa wengine kwa sasa, humkumbuka msichana mmoja kila anapotaka kuandika nyimbo za aina hiyo.

Si Wema wale ex wake mwingine unayemfahamu, Harmonize amemtaja baada ya mimi kumuuliza tetesi kuwa mashairi ya bosi wake huyo kwenye Bado, yalimlenga ex wake, Wema Sepetu.


“Diamond hajaanza kuimba leo mambo ya kuachwa, aliimba Kamwambie, akaimba Mbagala,” Harmonize amesema kwenye Chill na Sky.
“Mimi naamini kabisa, hata mimi mwenyewe nilivyomuuliza ‘kwani ulimuimbia nani Kamwambie?’ akasema mimi nikitaka kuandika nyimbo yoyote ya mapenzi namkumbuka Sarah mwanamke ambaye nilimpenda sana.”

Sikiliza Chill na Sky na Harmonize hapo chini.

Bongo5.com

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hamkumbuki Zari alombambikizia mtoto?

    ReplyDelete
    Replies
    1. JARIBU NA WEWE KUBAMBIKA KAMA NI RAHISI HIVYO. ACHA CHUKI WEWE MTOTO WA DIAMOND KAWAUMBUA BADO MKO KWENYE DENIAL .POLE WE

      Delete
    2. Anony wa 2.51 pm umejibu sahihi, mijitu mingine bwana imekalia maisha ya mtu utafikiri alipokuwa anambambika huyo mtoto alipewa yeye ampeleke kwa mond, acheni ujinga fanyeni yenu mwacheni mond na zari wake pamoja na tiffa wao mmeumbuka ndo maana mnaona aibu washenzi wakubwa

      Delete
    3. MWAMBIE HUYO WIVU WA KUPITILIZA UMEMZIDI. MTOTO MACHO DIAMOND MDOMO DIAMOND MASHAVU DIAMOND. ACHA WIVU WA KIJINGA,

      Delete
    4. kapime na wewe na baba yako uone kama ni kweli babako!!!

      Delete
    5. Mlipewa chance kumzalia kumbe mayai hamna sasa chokochoko za nini wakati mna undertaker ha ha ah aha

      Delete
  2. UKWELI LAZIMAAAAAAAAAAAAAAA USEMWE MAMBO YA TEAM TUPA KULEEEEEEEEEEEEEE TIFFAH SI DAMU YA MOND,KAMA PICHA YA KATUNZI UIJUI ITAFUTEEE MAPEMAAAAA UOANISHE NA PICHA YA TIFFAH.SISI WATANZANIA U TEAM UNATUFANYA KUSHIKIWA MAPEMBE KAMA MBUZI,ZARI KAMBAMBIKIA MTOTO KAOGOPA KUAIBIKA KUZAA NA MUME WA MTU AMBAE NI KATUNZI,MOND ANAJUA SANAAAAAA KWA TAARIFA YAKO ILA HAKUNA JINSI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. alaa kumbe anajua?

      Delete
    2. Tiffa Dangote hafanani na Katunzi hata kidogo ona mdomo wa Tiffa Dangote ni Diamond ndiyo baba wa Tiffa Dandote

      Delete
  3. Diamond anajua sana ila Hana la kusema kwa sababu kizazi kakiziba. Kwa kutaka utajiri!!!😆😆anajua Sanaa mtoto sio wake na mama yake pia anajua kutokana na ushirikina walio ufanya nyie muulizeni wema anajua mambo yoooteee!!!!zari yeye hajui chochote na alivyom bambikia mtoto akili yake anafikiri diamond hajuii!!!mxiuuu...wajinga ndo waliwaoo!!!hivi mnafikiri kwann diamond hataki DNA?

    ReplyDelete
  4. mimi nilijua tu Diamond anatumia ushirikina sababu hamna mwanamuziki yeyote aliyejenga jumba la kifahari bongo na anayesafiri sana mpaka kukutana na wasanii maarufu marekani kama Diamond huo unaitwa ushirikina mtu huwezi kufanikiwa namna hiyo bila nguvu za kishirikina na mambo ya kishirikina mwisho wake ni mbaya utakuja kufilisika na vitu vyote kuyeyuka na kujikuta mikono mitupu na watu kukusahau, muulize MR Nice

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad