Freeman Mbowe, Halipwi Mshahara Wowote na Chama Wala Posho

Baada ya wengi sana jana kuhoji mshahara wa mwenyekiti wa chadema .mh freeman mbowe kufuati mh rais kutaja mshara wake. HILI NDIO JIBU LAKE

Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe halipwi mshahara wowote na Chama. Amekitumikia Chama kwa kujitolea kwa zaidi ya miaka 20 akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu tangu aliposhiriki kuasisi Chama 1992, Mwenyekiti wa Vijana Taifa na baadaye Mwenyekiti wa Taifa kuanzia mwaka 2004.
Mbali na mshahara, Mbowe halipwi posho wala stahiki ya aina yeyote kama gari, nyumba, mawasiliano n.k na Chama. Utendaji wake ndani ya Chama ni wa kujitolea na kutoa.

Utamaduni huu umejengwa na viongozi wengi ndani ya Chadema kuanzia ngazi ya juu hadi chini. 

Wanaolipwa posho ni watendaji wachache wanaofanya kazi full time katika ngazi ya Taifa na Kanda. Wabunge na madiwani wote walio na wadhifa wowote ndani ya Chama au katika Mabaraza yake nao hujitolea kwa asilimia 100 kwa kila namna watendapo majukumu yao ndani ya Chama. Hawapokei mishahara wala posho mbili mbili. 

Hivyo Mbowe na viongozi wenzake wengi wa ngazi mbalimbali hawalipwi na Chama bali wao hukigharamia Chama kiweze kukua na kutekeleza majukumu yake kadiri iwezekanavyo.

Chanzo : Afisa habari Chadema
. Tumaini Makene

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama ni kweli hongereni sana

    ReplyDelete
  2. huongo mtupu akafanye kazi kanisani basi au msikitini kama kweli anajitolea .wanafiki wakubwa chadema.

    ReplyDelete
  3. hatujawauliza matumizi ya mishahara yao ila tunauliza ni kiasi gani wanalipwa

    ReplyDelete
  4. Ni upuuzi mtupu na uongo uliopitiliza mipaka. Kwanza kabisa hii inaleta taswira yakwamba chama ni mali yao na si waajiriwa wa chama. Mtu yeyote anaeitizama taasisi ya uma kama mali yake huishia kuwa dikteta. Na tumejionea wenyewe jinsi Mbowe alivyomleta lowasa kuwania nafasi ya uraisi kwa ticket ya ukawa na chadema ni kwa njia ya kidiktetaship . Hakuwa na mpinzani wala wagombea wengine hawakuruhusiwa kumchallenge pure dictatorship process yaani ni mauziano ya post kati ya mbowe na lowasa na baadhi ya wapambe wachache wa mbowe. Kiasi gani mbowe kavuta kwenye dili la lowasa? ni siri yake lakini tusifanywe wapumbavu wakuamini kama akina mbowe wanafanya bure chadema kwani Never can be something for nothing except there always be something for more things.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad