Fuvu la Binadamu Ndani ya Ofisi ya Mwanamuziki Diamond Platnumz...

Fuvu la binadamu lakutwa limewekwa kwenye meza ya Diamond pembeni ya picha ya mwanawe Tifah.
Diamond asema ni kweli ni fuvu la binadamu, ila ni pambo tu kama mapambo mengine, yeye anamtegemea Mungu.

Wakati mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii ndumba kwenye muziki wake ambao sasa umemfikisha mbali kimataifa, staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’, ameshikwa uchawi kufuatia kukutwa laivu kwa fuvu la binadamu ndani ya ofisi zake.

Fuvu hilo liko mkono wa kushoto mezani kwa Diamond huku jirani yake kukiwa na picha ya mwanaye, Latiffah Nasibu ‘Princess Tiffah’ iliyokuwa kwenye fremu.

Shuhuda mmoja aliyehudhuria hafla ya kusaini mkataba wa dili jipya alilosaini Diamond la Ubalozi wa Tomato Sauce ofisini kwake hapo alilithibitishia kuwepo kwa fuvu hilo lilozua gumzo kwa mashuhuda wachache wa tukio hilo.

“Ni kweli kuna fuvu la binadamu mezani kwa Mond (Diamond) but (lakini) sikufanikiwa kulishika kwa mikono yangu,”

Shuhuda mwingine aliripoti pia:

"Kuna ishu tumeishuhudia kwa macho yetu hapa ofisini kwa Diamond. Hata sisi imetushtua, ...hapa WCB, kwanza Diamond mwenyewe yupo. Ukifika ofisini kwake, tena kwenye meza yake (Diamond) mwenyewe kuna fuvu la binadamu kabisa.”

"Jamani ni fuvu la binadamu kabisa lenye mifupa. Inawezekana ndiyo chanzo cha utajiri wake na skendo inayomkabili ya uchawi katika kazi zake. Ninyi fuatilieni mtapata ukweli."

Mapema wiki hii, wageni mbalimbali waliofika kwenye ofisi za mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB), Diamond au Mond zilizopo Mapambano-Sinza jijini Dar, walitonya kuwa, wengi walishtushwa na fuvu hilo baada ya kuliona mezani kwa mwanamuziki huyo.

“Hata mimi nimelishuhudia hilo fuvu kwa macho yangu wala sijasimuliwa na nina picha zake kwenye simu yangu (huku akiperuzi kwenye smartphone). Kiuweli limezua sana minong’ono. Baadhi ya watu wanadai ni mambo ya uchawi na wengine wanasema ni moja ya alama ya Freemasons (jamii ya siri inayohusishwa na utajiri). Unajua fuvu la binadamu ni moja ya Alama za Freemasons na kama unavyojua Diamond amekuwa akitajwatajwa."

“Wapo wengine wanadai labda mambo hayo ndiyo chanzo cha utajiri wa jamaa (Diamond) wa
ghafla lakini yeye mwenyewe ndiye mwenye kuufahamu ukweli."

“Lakini unajua kunapokuwa na ishara kama hizi (kukutwa kwa fuvu) ni rahisi sana kwa mashabiki wake ambao ni wengi kuhusisha na huu utajiri wake unaotajwa kufikia (shilingi) bilioni nane kwa sasa,” alidai mgeni huyo.

DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya kupokea ushuhuda na madai hayo mazito ya Diamond kuhusishwa na uchawi na Freemasons kufuatia kukutwa kwa fuvu hilo ofisini kwake, gazeti hili lilimfuata Diamond ofisini kwake lakini alikuwa ametoka.

Alipotafutwa kwa njia ya simu alifunguka kwa kifupi huku akidai kuwa fuvu hilo ni pambo tu kama mapambo mengine.

“Ni urembo au pambo kama mapambo mengine, hakuna kitu kama hicho,” alisema Diamond na alipobanwa kueleza alikolitoa na gharama zake alisema:
“Usidanganyike, hakuna anayeweza kumuweka mtu juu zaidi ya Mwenyezi Mungu.

“Mimi naswali sana na namtegemea Mungu kwa kila kitu na kweli ananipigania.
“Unajua watu wengi wamekuwa wakizungumza oooh…natumia uchawi lakini ukweli ni kwamba maombi, ubunifu, juhudi na heshima ndivyo vitu vinavyoweza kumfanya mtu yeyote kupata mafanikio katika kitu akifanyacho au jambo alifanyalo.”

HUKO NYUMA
Mara kadhaa Diamond amekuwa akihusishwa na matumizi ya nguvu za giza katika kufanikiwa lakini amekuwa akisisitiza kuwa siri ya mafanikio yake ni kujituma, kutafuta fursa na kuipenda kazi yake ya muziki ili sanaa ya Bongo ifike mbali.

Chanzo:Global Publishers

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbona bado? mtaona mengi ya kishirikina. walikuwa wanafanya siri sasa wamenogewa imekuwa dhahiri.

    ReplyDelete
  2. sasa hilo fuvu ni la mwanadamu aliyekuwa akiishi wapi na alikufa lini!! na wamelitoa wapi makaburini au kwenye jumba la makumbusho la rwanda!!? maana zari kutwa kudhulu rwanda kwenye kumbu kumbu kumbe wana mambo yao!! pesa hizi lo shetani!!!

    ReplyDelete
  3. mbona toka zamani anatumia dumba? na mama yake ndo mshika hirizi zake sasa hataki kushuka mganga kamuongezea ndumba!

    ReplyDelete
  4. Diamond anatumia uchawi, kwani mwanamuziki wa kibongo hawezi kufanikiwa kimataifa bila uchawi

    ReplyDelete
  5. kafanyeni na nyinyi huo uchawi halafu muone km mtatajirika dai keep going achana na vumba la watu litakuchafua

    ReplyDelete
  6. ndio Dai ni mshirikina na mama yake ndo msiri wake. Vumba unalo wewe limekuganda mpaka matakoni Anony 11.14 AM.

    ReplyDelete
  7. HAKUNA UCHAWI WOWOTE NI JUHUDI UBUNIFU HESHIMA NA UAMINIFU. HONGERA DIAMOND MUNGU AKUZIDISHIE. WANAOSEMA WAACHE WASEMA USIKU WANALALA. HONGEZA BIDII

    ReplyDelete
  8. Kama wachawi wanachukuliwa sheria wakikutwa navn viungo vya binadamu na kwa nini Diamond asichukuliwi hatua za kisheria. Mimi najua ni kosa la jinai ukikutwa na kiungo cha binadamu.

    ReplyDelete
  9. kutumia uchawi ktk kazi kwa wabongo ni kawaida sana wala sio swala la kushangaza coz ndo imani ya watu wengi 90% ya wabongo ni wachawi..hivyo swez mshangaa sema tu kwa kuwa yeye ni star ndo maana kila mtu atazungumza yake hata wale wanaotumia pia NK

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad