Kuna tetesi kuwa Gerald Hando na Paul James aka PJ wanaelekea EFM baada ya kuacha kazi Clouds FM walikojizolea umaarufu kwenye kipindi cha Power Breakfast.
Hando, PJ na Barbara waliziba pengo la Masoud Kipanya na Fina Mango waliokuwa watangazaji wa kipindi hicho chenye wasikilizaji wengi kwa miaka kibao. Jana, kipindi hicho kiliwapa surprise wasikilizaji wake kwa kuwaleta tena Fina na Masoud, na kwa waliosikiliza kipindi hicho, watakubali kuwa mambo yalipendeza.
Swali ni kwamba wawili hao ndiyo wamerejea tena Clouds FM? Fina alikuwa na kipindi chake Magic FM kiitwacho Makutano, je kimekufa? Tunafahamu kuwa Masoud yuko available kwa sasa hivyo uwezekano wa yeye kurejea kwenye redio yake ya zamani ni mkubwa.
Wengine wanaamini kuwa wawili hao walifanya kipindi hicho tu na hawatarejea tena. Lakini kama wakirejea, basi ushindani kwenye vipindi vya asubuhi hasa ukizingatia kuwa PJ na Hando wataenda EFM, utakuwa mkubwa.
Gerald Hando na Paul James aka PJ Wanaelekea EFM Baada ya Kuachwa na Clouds FM....Kipanya na Fina Mango Je?
0
April 03, 2016
Tags