HALIMA MDEE Amshukia Rais John Magufuli...Amtaka Ataje Marupu rupu na Posho Anazopata Tujue Jumla ya Mshahara wake

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.

Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi, uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.

Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.

Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee.

Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.

Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.

Mbunge wa Jimbo la Ndanda katika Wilaya ya Masasi, Cecil Mwambe alidai katika mkutano huo kuwa wananchi wa Mtama wamekosa mwakilishi wa kuwasemea matatizo yao, hasa ya upande wa kilimo cha korosho kutokana na mbunge wao, Nape Nnauye kukosa uwezo wa kusimama bungeni kuisema Serikali.

Mtama mmekosa mwakilishi, hapa kuna tatizo la korosho na mbunge aliyepo anashindwa kulisemea, hivyo mtabaki hivyo hivyo bila kutatua tatizo lenu kwa kipindi cha miaka mitano,” alidai Mwambe.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbona haseme na mbowe mshahara wake

    ReplyDelete
  2. Halima husikilizi habari?Tingatinga kasema akirudi likizo atadadavua kila kitu kuhusiana na mapato yake,mwambie na Mbowe sasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli hasikilizi habari kazi kuropoka hvy tuu tuu
      huyu dem atafute tuu bwana aolewa manakee ni ziro kabisa

      Delete
    2. Unasema aolewe?? Ataolewa vipi wakati yeye mwenyewe msagaji, anamsaga Ester Bulaya

      Delete
  3. Chadem ndo basi ten yaani wanakos sabab zozot za kumchafua rais alaf wanaanza kugangania mshahar wak hiy ni aibu kwa cham chaupinzan. Waachan na upinzan wakuoz na wafany mamb muhim wakuwatumikia wanainchi sio kulet hoj za mifupa. Bunen mbin mpya na zamana kwa ajili yakuwatumikia raia sio kuwafuatilia fuatilia watawal kwanz nyiny wabung waupinzan hiz pes mnapokea mwisho wamwez si zabur tu wakat hamufanyii wanainch chochot?

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni mbunge wng lakin dah simwelewi kabisa

      Delete
    2. i hate this dude angalijua navomchukulia basi yaani ni mwanamke dume sauti mbaya

      Delete
  4. Kwa kazi anazozifanya JPM, mpaka hapa tulipofika, hata angesema analipwa mshahara sh. millioni 200 kwa wiki, ingekuwa poa tu!! TUMEMKUBALI, HAPA KAZI TU........

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jamani!Hata mimi na upinzani wangu lakini kwa JPJM napiga POO!TUMUOMBEE TU BASI,MAANA WAKO WENGI HAWAPENDI HAYA ANAYOYAFANYA NA HASA KUTUMBUA MAJIPU.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad