Hemed PHD: Sitaacha Kujipodoa kwa Hofu ya Watu

MWIGIZAJI wa filamu na msanii wa Bongo Fleva, Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’, amesema kwamba hataacha kutumia vipodozi kwa kuwa humuweka nadhifu na humwongezea mvuto wa mwili wake.

Hemed anayetamba na wimbo wake wa ‘Imebaki stori’, alisema vipodozi anavyotumia zaidi ni poda, lipshine na pafyum na hataacha kujiremba.

“Sitaacha kujiremba kwa sababu kujiremba siyo kwa wasichana tu hata wanaume tunatakiwa tujipake vipodozi, kama poda na lipshine zinasaidia kuongeza mvuto na mwonekano nadhifu zaidi, mimi ni staa natakiwa niishi kistaa hivyo vipodozi ni kitu cha kawaida.

“Mara nyingi vipodozi navitumia nikiwa katika kazi zangu ili nionekane tofauti nyumbani na kazini hivyo nasisitiza kwamba siwezi kuacha kupaka vipodozi kwa kuogopa maneno ya watu,” alimaliza Hemed.

Mtanzania
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani nani anakukataza? Wewe chakula fanya utakalo ataukitaka kuingia mashindano ya miss tanzania rukhsa, mwanamke we

    ReplyDelete
  2. Hata ukitaka kuolewa pia tupo waume shenz.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad