Hii tumbua tumbua majipu ya Rais John Pombe Magufuli, japo inafanyika kwa nia njema, swali la kujiuliza ni Jee mtangulizi wake, Jakaya Mrisho Kikwete anajisikiaje?!.
Kwa jinsi Magufuli anavyotumbua baadhi ya majipu, kunamuabisha sana mtangulizi wake, Jakaya Kikwete kumfanya Kikwete kuonekana kuwa alikuwa ni rais dhaifu sana, kiasi cha kulea madudu kibao, as if awamu ya JK kulikuwa hakuna lolote la maana lililokuwa likifanyika zaidi ya kulea uzembe, as if serikali ya JK ilikuwa ni serikali goi goi, kazi yake ilikuwa ni kulala tuu usingizi, lakini sasa awamu hii ya Magufuli, "hapa kazi", ndio serikali sasa inafanya kazi!.
Just imagine kama wewe ndio JK, unaposafiri unakutana na ma diasfora wa Tanzania kwenye nafasi nzuri ughaibuni, huku wanalipwa vizuri, unawaomba warudi nyumbani kuja kuutumia ujuzi wao kuijenga nchi, baadhi ya wana diaphora hawa wanaguswa na uzalendo, wanakubali kurudi nyumbani na kuukubali umasikini wetu, lakini wanakuwa wakweli kuwa mishahara ya seikali ni midogo mno kuwavutia kurejea nyumbani, JK unawabembeleza na kuwaahidi utajitahidi kuwaongezea kidogo katika kugawana umasikini, japo hautawalipa kama wanavyolipwa huko ughaibuni, lakini utaboresha boresha zaidi angalau kufikia kiwango cha kumfanya asurvive comfortably, hivyo baadhi yao wanakubali wanarejea nyumbani.
Kwa vile wamekuja kwa promise, wanaamua kutopokea any less than the promised amount, wewe unamuahidhi kufuata taratibu za kufikia kiwango kilichoahidiwa, sasa hata kabla muafaka haujafikiwa, mtu aliyekufuatia uliyemkabidhi kijiti kwa upendo wote, kazi yake ya kwanza ni kuwakomoa baadhi ya wateule hawa!, Magufuli alianza na Bade pale TRA, wakafutia wengine, na jana ndio ilikuwa zamu ya Juliet wa TIC, jee ungekuwa ni wewe JK, utajisikiaje?!.
Anachokifanya Magufuli, is it fair kwa JK, kuwatimua watu wake kwa kuwakomoa, jee anawakomoa hao anaowatumbua, au anamkomoa JK na kumuaibisha kuwa JK alikuwa dhaifu mno, hadi kushindwa kuyatumbua hayo anayoyaita majipu?!.
Jee kuna uwezekano kuna baadhi ambao hawakumchagua Magufuli, (walimchagua yule 'jamaa yetu') lakini sasa wanamfurahia Magufuli kutokana na huu utumbuaji wa majipu, lakini kuna waliomchagua Magufuli, akiwemo Kikwete na wote waliotumbuliwa, ambao kutokana na nyadhifa zao, lazima walimchagua Magufuli, lakini sasa wanajuta?!.
Hii tumbua tumbua ya majipu, imekuwa popular hadi kubadili majina ya watu, wale wote waliotumbuliwa, hawatajwi tena kwa majina yao, bali sasa wanaitwa "jipu", hata majirani zao wanawaona kama ni majibu!, mtu unajitolea kuacha maslahi bora ughaibuni kwa kusukumwa na uzalendo, na kuamua kurejea nyumbani, kuitumikia nchi yako kwa moyo wa kujitolea tuu, mara ghafla unatumbuliwa!, hata jina unabadilishwa unaitwa "jipu", is this fair kweli?!.
Kama JK bado anajisikia proud kumkabidhi nchi Magufuli, kwa haya anayoyafanya na kwa stahili hii, ikiwemo uonevu na kuaibishana, then JK ndio mwenye matatizo!.
Imeandikwa na Pasco
Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete Anajisikiaje?...Anajisikia Sifa Au Anajuta?
7
April 29, 2016
Tags
km ni majipu yameshatumbuliwa sana, tunachotaka watanzania ni kuona unafuu wa maisha sukari imeshapanda bei, sio hiyo tu bidhaa zote za kawaida na chakula rais tunakuomba angalia haya kwanza hali ni mbaya sn
ReplyDeleteTulia weweeee mtaongea yote sahv hatuangalii sura wala ulikaa ughaibuni ukarudi kama una madudu yako fungasha virago unaona tz hapakufai rudi ulikotoka Raisi atatumbua yani mpaka majipu yaishe mdogo mdogo tu..anaeona anadhalilishwa achape lapa huko ughaibuni alikotoka...hii ni tz ya majipu na yatatumbuliwa mtake msitake mcheke au mlie ndo hivyo ishakuwa
ReplyDeleteJK is in shock! Yaani Magufuli akivyokuwa anamuenzi JK, inashangaza kuona sasa hataki mtu wake hata mmoja.
ReplyDeleteAccording to report, Kariuki salary in South Africa was $1500 a month. At TIC she paid herself 10 days overseas monthly travel allowance amounting to 400,000/- ($181,900)from special fund set up for investors. Even worse she defended Dangote against TRA when TRA requested Dangote to pay tax; guess what Dangote makes payment to the special fund in which Kairuki withdraws her allowances. In respect of Bade we all know what happened under his leadership. These people you are defending just because they are diasporas who gave up their positions overseas due to patriotism apart from causing loss of income to the nation what good have they done. I am diaspora residing in Australia, my monthly income is $7000 do you think I will be that mad to be lured to take presidential appointments such as Bade's and Kairuki's in Tanzania? my current position is secured. What I,m trying to say is that they were not patriots as it seems, they took the positions because they new they will make quick bucks; there is not patriotism in that
ReplyDeleteWee anonymous wa Australia yr numbers do not add up.
ReplyDeleteHawezi kukaa bila kupokea mshahara.yeye mwanasheria ni mjanja.kuna sehemu anapata hela za hongo.ni hawa dhaifu waliopewa kaxi na Kikwete kwa kiurafiki wakishirikiana kuiibia Tanzania kijanja. Hapa namhisi Kikwete ameshiriki moja kwa moja kuibia mchi hii.aliwaleta wale week people na kipitia hao amejihusisha moja kwa moja kuitafuna nchi kwa upangilio wa hali ya juu.Namhisi Kikwete pia namshukia kupitia Dangote.huenda anamalupulupu huko.hii nchi imetafinwa kwa mahesabu na mipangilio n mbinu za hali ya juu. Magufuli laxima umtumbue Kikwete.
ReplyDeleteHii Tabia ya kuitafuna nchi ndio maana hatuendelei, tutaendeleaje uchumi unatiwa mifukoni na watu wachache kama wao ndio wenye nchi pekee yao?,Hasa bara hili la Afrika lina viongozi wabovu ni hakuna mfanowe yaani ni shida, afadhali hata raisi wetu mpya Magufuri anajali mustakabali wa Taifa kushinda hao waliipita ni shidaa,
ReplyDelete