Kocha wa Toto Africans John Tegete amesema timu yake inacheza soka linaloshabihiana na la Simba kwa kiasi kikubwa lakini wachezaji wake wananguvu na ndiyo siri ya kuichapa Simba katika mchezo wao wa Jumapili.
Simba imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Toto na kuziachia pointi tatu muhimu ambazo kama wangezipata zingewapandisha kileleni mwa ligi na kuipiku Yanga kwa ponti moja mbele.
“Mfumo wanaoutumia Simba ndiyo tunaoutumia sisi kucheza, wao wanapenda kuchezea mpira na sisi tunapenda kuchezea mpira lakini sisi tunawazidi ujanja kwasababu sisi tunafanya mazoezi ya nguvu kwasababu wachezaji wetu wananguvu za kutosha. Wachezaji wa Simba hawana nguvu ndiyo maana tunawafunga”, anasema John Tegete ambaye ni baba mzazi wa mshambuliaji wa Mwadui FC Jerry Tegete.
“Wachezaji wangu wamefanya kazi niliyowatuma mchezo huu ulikuwa kama fainali kwetu kwasababu tulikuwa tunajua tunacheza na timu yenye jina kubwa, siyo timu timu kubwa kwasababu timu zote zipo sawa zote zipo kwenye Premier League”.
“Mchezo wetu dhidi ya Simba ndiyo ulikuwa unaamua kama tunabaki kwenye ligi au tunashuka daraja, lakini tumedhihirisha kwamba bado upo kwenye ligi na ndiyo maana wachezaji wangu wanafurahi”.
Simba wameambulia pointi moja msimu huu kutoka kwa Toto kufuatia kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ulichezwa jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kupoteza mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa taifa na kuichangia pointi nne timu hiyo kutoka mwan
piiiiigaaaaaaaa wamchangani hayooooooooooooooo!!!!
ReplyDeleteSasa wasubiri kunyolewa sharubu zao na wembe butu wa AZAM.
ReplyDelete