Ishu ya Kubwia Unga, JK Amuonya Mwanamiziki Ray C

Wakati msuguano mkubwa ukiwa umeibuka, Mbongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akisukuma madongo kwa Magazeti Pendwa ya Global Publishers kwamba yanamtungia uongo kuhusu hali yake ya kurejea kubwia unga akisema hayuko hivyo kwa sasa, kuna taarifa kwamba, Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ amemuonya kuhusu kutozingatia matumizi ya dawa za methadone.
Methadone ni dawa zinazotumiwa na waathirika wa matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’ ambapo Ray C anatumia kwenye Hospitali ya Mwananyamala, Dar baada ya kuathirika.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini hospitalini hapo, Ray C alipata onyo hilo baada ya Magazeti ya Global kuandika kwamba nyota huyo amerejea kwenye kubwia unga huku akiendelea na methadone, hali ‘inayomzimisha’ mara kwa mara.

“Jamani nataka kuwaambia, mnajua mlipoandika kwamba Ray C karejea kwenye unga wakati akiendelea kutumia methadone, JK alisoma, akamtumia ujumbe akimtaka ajiangalie kwenye kukazana kutumia dawa na kuachana moja kwa moja na matumizi ya unga.
“JK amemtaka aangalie mwenendo wake kwa sasa. Yaani bwana sijui vipi, JK anamtakia mema  lakini yeye hajijui tu.

“Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba juzikati Ray C alikuja pale Hospitali ya Mwananyamala (jijini Dar), akawaangukia madaktari wake wanaomtibu akiwaomba msamaha kwamba amekuwa akiwapuuza katika ushauri lakini amegundua wao ndiyo msaada mkubwa kwake,” kilisema chanzo hicho.


Kitendo hicho kinatokana na madaktari hao siku za karibuni kumshindwa staa huyo katika kumpa mwongozo wa matumizi ya dawa hizo, hivyo kuamua kumrudisha nyumbani kwao, Bunju, Dar

Taarifa zaidi zinasema kuwa pia baada ya Magazeti ya Global kuandika habari ya anayemmaliza Ray C ni kijana Frank, ndugu zake wamemfuata na kumrudisha nyumbani kwao, Arusha.
“Unajua ndugu zake walikuwa wakimtafuta, alipotoka kwenye gazeti wakamwona, wakamfuata Mwananyamala kumchukua,” kilisema chanzo.

Utafiti uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa ile ‘posti’ ya Ray C aliyoitupia kwenye mtandao wake wa Instagram mara baada ya kuandikwa na Gazeti la Ijumaa Wikienda la Machi 28, mwaka huu, habari ikiwa na kichwa; RAY C ANASWA AMEZIMIKA, akitoa shutuma nzito kwamba picha zile si zake bali ziliungwaungwa, ameifuta!

Udadisi zaidi unasema kuwa kufutwa kwa posti hiyo kunatokana na Mbongo Fleva huyo kuguswa na dhamira yake huku pia michango ya wafuasi wake waliojitokeza kumwandikia ukweli kumwambia, picha zile ni yeye na hakuna aliyeziunga!

Ray C alipotafutwa juzi ili kujibu madai hayo alikosekana hewani licha ya kupigiwa simu mara kwa mara kwa siku nzima.

Chanzo:Global Publishers
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. RAY C,RAY C,
    JAMANI TUMESHACHOKA,MWACHENI TU AZIMIKE MOJA KWA MOJA,
    KWANI KUNA HASARA GANI?

    ReplyDelete
  2. maombi ndiyo yatamsaidia na akubali kumpokea Yesu atavuka anayeweza kumbadilisha ni Mungu tu

    ReplyDelete
  3. Who is ray c???!! Mwcheni wangapi wanapoteza uhai kwa sababu hizohizo,tunajua kila mtu ataonja mauti, bc nae aendelee tu hatudanganyi cc bali afya yake

    ReplyDelete
  4. Wabwia huwo unga wamejaa kibao hapa, sio Ray c ti. Kama kusaidiwa wote wasaidiwe na

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad