Kabwe Asema Uchunguzi Ufanyike ili Kubaini Ukweli, ni Baada ya Kutumbuliwa

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa tuhuma zilizomfanya Rais John Magufuli kumsimamisha kazi jana utabainisha ukweli wa tukio hilo.
kabwe

Alisema hayo mara baada ya Dk Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni ambalo sasa litaitwa Daraja la Nyerere baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza tuhuma dhidi ya mkurugenzi.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Jumanne hii, Kabwe alisema hakuwa na taarifa za kusimamishwa kwake na kama imetokea hivyo ni sawa kwa kuwa Magufuli ni mkubwa wake.

“Nimekwambia sina la kukwambia kwa sasa lakini nimesema tu sina shida na hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu. Lakini kama ukijulikana na ikibainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote nitalipwa?,” alisema Kabwe.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Jumanne hii alimlaumu mkurugenzi huyo kwa mambo kadhaa ya kiutendaji ikiwemo kuongeza mkataba wa maegesho ya magari kwenye jiji na ulanguzi wa kodi za mapango kwenye stendi ya mabasi ya Ubungo
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hivi pccb hamana mpaka rais anachukua hatua majukwaani, mawaziri, polisi na mahakama zipo wapi. mhhh

    ReplyDelete
  2. WEWE NAWE NI WA KUKATAA KWELI?HAYA NGOJA TUSUBIRI.

    ReplyDelete
  3. Pole bwana mkubwa nafasi ya kuonekana kuwa umusafi ndogo sana maaana hata madudu uliyo yafanya mwanza sasa yenyewe yamewekwa hadhalani yani wewe jiandae na safari ya likizo huko segerea hahahahaa Magufi kweli kiboko yaooo

    ReplyDelete
  4. 2020 huitaji kufanya campaign tumekupaaa tayari tick.

    ReplyDelete
  5. Hamna muda wa kutafuta uchunguzi kwa huyu mjinga mmja , ni mengi aliyoyafanya kwa wizi dawa yake ni mmja ni kutumbuliwa tena kwa herufi kubwa, kwa kuwa anajipu kubwa tambaza, aende tu uraiani, hawa ndio watu corrupt, wanaotunyima maendeleo ya kukosa huduma nzuri na miundombinu mizuri hapa nchi kwetu kwa kujaza mifuko yako kwa hela zetu za kodi, akajambe mbeleee kule, uk

    ReplyDelete
  6. Mmm huyu kwa utajiri alio nao hata hao akina Mengi wanaweza kuwa cha mtoto.Mungu wetu asante kwa kuanza kuikomboa TZ

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad