Lugumi Enterprises ni kampuni iliyoandikishwa na kufanya kazi hapa Tanzania na imekuwa ikifanya kazi mbalimbali ikiwemo ununuzi na ufungaji mashine za utambuzi wa alama za vidole yaani Automated FingerPrint Information System (AFIS)
Hivi karibuni kumekuwa na habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa namna ambayo inapotosha ukweli kuhusu kampuni yetu iliyotekeleza mradi huu muhimu kwa nchi yetu na, mradi wa AFIS.
Aidha taarifa hizo katika mitandao na magazeti mbalimbali imekuwa ikitoa habari zisizo na ukweli wowote kuhusu mtendaji mkuu Bwana Said H. Lugumi.
Ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2011 Jeshi la Polisi liliingia mkataba na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited wa kufunga mitambo ya utambuzi kwa kutumia alama za vidole (AFIS) katika vituo vya Polisi kwa mujibu wa matakwa ya Jeshi. Vituo vilikuwa nchi nzima Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za kampuni yetu, ukweli ni kwamba mkataba huu umetekelezwa nasi kwa kushirikiana na wabia wetu katika kuhakikisha mkataba huo unatekelezwa ipasavyo.
Kwa mujibu wa mkataba, kama kuna mgogoro katika utekelezaji,upande usioridhika na utekelezaji wake, utatangaza mgogoro kwa mwanasheria mkuu.
Si jeshi la polisi kwa upande mmoja wala sisi kwa upande mwingine aliyetangaza mgogoro wowote dhidi ya mwingine,kwa mujibu ya matakwa ya mkataba.
Kwa mantiki hiyo basi, mambo yaliyo mengi yalitajwa katika vyombo vya habari si ya kweli na ni upotoshaji mkubwa na ni muhimu kuyapuuza, na kuendelea na shughuli za kawaida za ujenzi wa taifa.
Ni katika muktadha huo huo tunapenda kuujulisha umma kwamba tuhuma nyingi za uzushi zimetungwa kumwelekea Mtendaji Mkuu Bwana Said H. Lugumi ikiwemo kuzushiwa kutoroka na kukamatwa nje ya nchi na kadhalika.
Taarifa hizo ni uzushi mtupu, ni za kupuuza, Mkurugenzi wetu yuko nchini na anaendelea na shughuli zake za kawaida.
Imetulazimu kuandika na kueleza haya maana tumeona vyombo vya habari vimezidi kuandika na kupotosha umma kuhusu jambo hili.
Kampuni ya Lugumi Yajitokeza na Kusema Mkurugenzi wake Hajatoroka nchi.....Bofya Hapa Kuisoma Taarifa Yao
0
April 20, 2016
Tags