Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji Amemtaka Rais Magufuli Apunguze Utumbuaji Majipu


Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amemtaka Rais Magufuli apunguze utumbuaji majipu. Adai inadhalilisha Watumishi wa Serikali

Alisema pamoja na kuwa CHADEMA wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawako tayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi. “Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji. “Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.

Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake. “Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani lakini niwaulize sukari imeshuka bei au mchele umeshuka bei lakini kila siku tunasikia watu wametumbuliwa bila kuwa na tija kwa taifa,” alisema.

Aliwataka vijana wa vyuo vikuu nchini kuungana na CHADEMA katika kuhakikisha serikali inaruhusu kuonyeshwa kwa vipindi vya Bunge moja kwa mpja kama ilivyo kuwa hapo awali.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Rais wetu mpendwa endelea na utumbuaji hapa kazi tu

    ReplyDelete
  2. wewe katibu mimi mwenyewe upinzani lakini naona unaongea utumbo,cha muhimu ni kumsampoti raisi na kushinikiza katiba ibadilishwe.

    ReplyDelete
  3. Kweli Ngoma nzito ukiona CDM wanatetea majizi ujue walikuwa wakipata ruzuku kutoka kwa haya majizi haiwezekani kwa hapa nchi ilipofikia mtu analeta siasa za utumbo eti kutumbuliwa majipu huku ni udhalilishaji huku wanaunga mkono unafiki usio kadirika tobaaaaa hata hawana haya utumbuaji wa majipu na sukari wapi na wapi kama CDM

    ReplyDelete
  4. Hivi huyu ndio Katibu mkuu mpya wa Chadema hajabadili kitu kwani staili ile ile waliyokuwa wakiitumia CDM ya kutafsiri matukio ya serikali toka enzi na enzi kama ni mfumo muanze nyinyi badilishene njia mbadala wa kuikabili serikali sio kila siku mambo yenu ya kihuni kuleta hoja za matukio wachane Magufuli asafishe uozo mgeshika nyinyi nchi ingekuwa ya Firauni afadhali ya Musa

    ReplyDelete
  5. Kuna viongozi walioshindwa kusimamia kazi ndio majipu makuu.kwa miono yangu hayo yabgetumbuliwa kwanza.hawa viongozi wa chini waliwafuata na kuwaiga wakuu wao.wakachukua chao mapema kama kawaida ya wanaccm Mtu wa juu aliyeshindwa ni Raisi wa mwisho mstaafu.kwa miaka kumi amewachia watu waifilisi Tanzania.Aliyaachia huru watu walioiba nabilioni wa ESCROW,na watu wa lptl hawa wameisababishia nchi hasara ya mabillioni.hawa utawatumbua lini. Raisi aliyepita pia alisema anamajina ya watu hamsini, hakuwataja je huyu sio jipu kuu aliyeiacha nchi iliwe na kuwakumbatia wahusika bila kuwafanyia kazi. Unawaacha majipu makuu au unawawekeza mwicho?.

    ReplyDelete
  6. kimya kingi kina mshindo mkubwa
    mzee kukaa kimya kote uko unakuja na kuongea pumba bora unge kaa kimya tuu

    ReplyDelete
  7. Nawaonea huruma wapinzani kwani hata Katibu wao hana point kweli anakuja kuwatetea wahalifu ni bora Mungu alitunusuru UKAWA hawakushinda Uraisi tungeharibikiwa
    Bungeni kazi yao ni kuzomea na kupiga kelele na kuburuzwa nje na polisi na bado wanadai wananchi waliowachagua waonyeshwe upuuzi wao LIVE kweli hawa ni pumba tupu

    ReplyDelete
  8. Ama kweli upenzani nchini unaondoka. Ivi huyu ndo katibu wa chama tunachotarajia siku moja kije kiendeshe nchi hapa kwetu. Kwa upinzani huu sitarajii kushika dola milele endapo hawatobadilika.

    ReplyDelete
  9. Ama kweli upenzani nchini unaondoka. Ivi huyu ndo katibu wa chama tunachotarajia siku moja kije kiendeshe nchi hapa kwetu. Kwa upinzani huu sitarajii kushika dola milele endapo hawatobadilika.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad