Baada ya Kutumbuliwa Jipu Laivu Darajani na Magufuli..Mkurugenzi wa Jiji La Dar es Salaam Wilsoni Kabwe Asema Haya...

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa tuhuma zilizomfanya Rais John Magufuli kumsimamisha kazi jana utabainisha ukweli huku akihoji; “ikiwa itabainika kwamba nilionewa nitalipwa fidia?”

Alisema hayo mara baada ya Dk Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni ambalo sasa litaitwa Daraja la Nyerere baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza tuhuma dhidi ya mkurugenzi.

Alipoulizwa jana, Kabwe alisema hakuwa na taarifa za kusimamishwa kwake na mazungumzo yake na mwandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwandishi: Habari mkurugenzi?
Kabwe: Salama.

Mwandishi: Tumepata taarifa za kusimamishwa kwako kazi na Rais kutokana na tuhuma zilizotolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda tunaomba maoni yako. Kabwe: Sijasikia ndiyo kwanza unaniambia wewe, kasema lini Rais?

Mwandishi:Leo wakati akizindua Daraja la Kigamboni. Kabwe: Alitamka palepale au?

Mwandishi: Ndiyo.
Kabwe: Sasa kama ameshasema yeye ndiyo mkubwa mimi sina la kusema tena.

Mwandishi: Nataka kujua unazungumziaje uamuzi huo? Kabwe: Nimekwambia sina la kukwambia kwa sasa lakini nimesema tu sina shida na hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu. Lakini kama ukijulikana na ikibainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote nitalipwa?
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hilo wala usiwe na wasiwaasi nalo..uuchunguzi WA kina tunaenddelra nao na ikibidi tutakufikisha mbele ua sheria na tukishindwa kuptove tutakulipa kukuharibia jina na malipo halali unayosyahiki..lakini ikithibitika juu yako jua ban inazilipa ulizokomba na tuna taifisha Mali zako zote na hats zile ulizo andikisha wake...halafu unaenda nya Debe..Kumbuka Makonda Yuko kibaruani na wasaidizi wake..na BABA JPJM anaangalia maendeleo yetu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad