Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ilianza kwa ajenda kubwa ya kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ambapo iliipangia Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ kufikia kiwango cha TRILIONI 12.363 kwenye makusanyo yake kwa mwaka 2015/2016.
April 04 2016 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Alphayo Kidata ametoa ripoti inayoonyesha kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha March 2016 kwa kukusanya TRILIONI 1.316 ambayo ni sawa na 101.0% ya lengo la kukusanya shilingi TRILIONI 1.302.
Jionee makusanyo kuanzia December 2015 mpaka kufikia March 2016 kwenye hii orodha hapa chini…….
Lengo
(Trilioni) Makusanyo halisi
December 2015 1,346,690.4 1,403,189.8
January 2016 1,059,863.9 1,079,993.2
February 2016 1,028,379.4 1,040,620.8
March 2016 1,302,482.3 1,316,072.4
Jumla ya makusanyo hadi sasa kuanzia mwezi July 2015 ni TRILIONI 9.88 ambayo ni 99% ya lengo la makusanyo ya TRILIONI 9.98 ya miezi tisa kwa mwaka wa fedha 2015/2016