Wiki iliyopita zilianza kusikika taarifa mbalimbali kuhusu kuhukumiwa kwa mpenzi wa zamani na mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili jijini Mwanza.
Pamoja na taarifa zote hizo kutoka hakukuwa na taarifa za kina kueleza ni nini hasa kilitokea mahakamani mpaka akahukumiwa jela miaka miwili ila taarifa za awali zilidai kwamba amehukumiwa kwa sababu ya kutukana mtu mtandaoni.
Wakili wa serikali Moris Mtoi ameongea kwenye exclusive interview na DStv na kusema ukweli au chanzo cha Siwema kuhukumiwa hakikua kumtukana mtu mitandaoni bali kumtishia mtu.
Amesema kilichompeleka Siwema jela nikumtishia mpenzi wake wa zamani kutoa picha za uchi walizopiga, Siwema alikua akimtishia kwamba asingetoa pesa na kumnunulia gari au kufata maagizo yake angezisambaza picha hizo kwa mke wake na watu wengine.
Wakili huyu wa serikali na mwendesha mashtaka kwenye kesi hii amesema vitu vingine alivyokuwa akivitaka Siwema ni kununuliwa nyumba na boyfriend wake huyu wa zamani.
katishia tu na wala hakufanya anahukumiwa miaka miwili walio fanya live wapo na walionekana hawana hatia kweli Tanzania ukiwa huna hela na huna jina unaonewa wanyonge wanateseka sana hakuna haki wala sheria.
ReplyDeletekweli wewe ni mtanzania mpumbavu na mbumbuu
Deleteshetani mkubwa wew unatetea dhambi ebu fatilia kisa kizima cha ushenzi wa huyo demu ujue
Acha kumtetea,hujui kutishia ni kosa?jiulize je angepewa hivyo vitu alivyotaka angekataa na kusema alikua anatishia tu?
ReplyDelete