Kilichomfanya Siwema wa Nay wa Mitego Afungwe Miaka Miwili Gerezani ni Kutishia Kusambaza Picha za Uchi za Mpenzi Wake


Wiki iliyopita zilianza kusikika taarifa mbalimbali kuhusu kuhukumiwa kwa mpenzi wa zamani na mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili  jijini  Mwanza.
 

Pamoja na taarifa zote hizo kutoka hakukuwa na taarifa za kina kueleza ni nini hasa kilitokea mahakamani mpaka akahukumiwa jela miaka miwili  ila taarifa za awali  zilidai kwamba amehukumiwa kwa sababu ya kutukana mtu mtandaoni.


Wakili wa serikali Moris Mtoi ameongea kwenye exclusive interview na DStv  na kusema ukweli au chanzo cha Siwema kuhukumiwa hakikua kumtukana mtu mitandaoni bali kumtishia mtu.


Amesema kilichompeleka Siwema jela nikumtishia mpenzi wake wa zamani kutoa picha za uchi walizopiga, Siwema alikua akimtishia kwamba asingetoa pesa na kumnunulia gari au kufata maagizo yake angezisambaza picha hizo kwa mke wake na watu wengine.


Wakili huyu wa serikali na mwendesha mashtaka kwenye kesi hii amesema vitu vingine alivyokuwa akivitaka Siwema ni kununuliwa nyumba na boyfriend wake huyu wa zamani.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. katishia tu na wala hakufanya anahukumiwa miaka miwili walio fanya live wapo na walionekana hawana hatia kweli Tanzania ukiwa huna hela na huna jina unaonewa wanyonge wanateseka sana hakuna haki wala sheria.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli wewe ni mtanzania mpumbavu na mbumbuu
      shetani mkubwa wew unatetea dhambi ebu fatilia kisa kizima cha ushenzi wa huyo demu ujue

      Delete
  2. Acha kumtetea,hujui kutishia ni kosa?jiulize je angepewa hivyo vitu alivyotaka angekataa na kusema alikua anatishia tu?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad