Kinachoendelea Afrika ya Kusini na Kiwe Funzo Kwa Nchi za Bara la Africa...Rais Afikishwa Mahakamani....

Kinachoendelea Africa ya Kusini na kiwe funzo kwa nchi za Bara la Africa,Huenda karata ya upinzani ya Nchi hiyo isifanikiwe kwasasa,ila Ilifanikiwa hapo awali baada ya kumpeleka Rais Mahakamani na Upinzani kuibuka kidedea.

Taifa langu Tanzanzia tunahitaji katiba mpya itakayoruhusu Rais kupandishwa kizimbani kwa kutumia mamlaka vibaya (Kufuja mali za umma) mambo ya kuwafanya marais kuwa ni watu wasiyogusika ni mambo ya kikoloni sana.
Tuitafuteni haki ya kupata katiba mpya itakayo wawajibisha Marais ama wakiwa madarakani ama nje ya Madaraka.

Vile vile tuwe na Katiba itakayomfanya Rais kuwepo bungeni na siyo utaratibu wa Sasa Wa Rais kulihutubia Bunge kisha mambo mengine yote anamuachia Waziri mkuu, Hapa hatuwafanyii Wananchi mazuri,Kumbuka Waziri huyu alichaguliwa na jimbo moja sasa anakuja kujibu Maswali ya nchi nzima....Tubadili muelekeo wa kisiasa kama tunataka kuwaletea Watanzania maendeleo na siyo maigizo ya kisiasa.

Kwasasa ni lazima waliyopo madarakani mkubali kupoteza vitu fulani na kuongeza vitu fulani vyenye manufaa kwa Wananchi....
TUITAFUTENI KATIBA MPYA

Written by Henry Kilewo

DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG HAPA
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wengine si wanatabia ya kumnyenyekea rais, hata na kumusudisha kama mungu mtu, na kumwita mtawala baadala ya kiongozi, hata kama raisi anaiba, anafanya ufisadi kwa mikataba ya uongo uongo, wao wapo tu, mpka unakuta raisi na kundi lake ni wezi wakubwa katika nchi, lakini mijitu ipo eti ni raisi, harusiwi kumshitaki, mpka na watoto wake na familia yake wote wanakuwa matajili, kwa wizi, lakini wapi?, hizi ndio tabia zetu za nchi nyingi za Africa, maraisi ni matajili na watoto wao na familia zao wamejijazia na mimali. Na mihela ya wizi kwenye mabenki ya kigeni, na kujimilikisha mauchumi ya nchi, yaani hao ndio viongozi wa bara hili na hapo hapo wanaudumiwa kila kitu na familia zao, bora mambo yawe hivi ni kumpelekana mahakamani na kufungana kila atakaye iba na kujilimbikizia mpka

    ReplyDelete
  2. Apo umesema mwandishi big up.

    ReplyDelete
  3. Apo umesema mwandishi big up.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad