Kisa Mil.98 Wema Sepetu Ammwaga Idris Sultan..Sababu zingine zatajwa pia zipo Hapa

Habari ya mtoto mzuri Wema Sepetu ‘Madam’ kumwagana na mpenzi wake, Idris Sultan si ngeni masikioni mwa wapenda ubuyu, imetapakaa kwenye mitandao ya kijamii lakini Amani limenasa sababu kubwa inayodaiwa kusababisha penzi hilo kuvunjika, twende pamoja.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, wawili hao waliripotiwa kumwagana rasmi ambapo haikubainika mara moja sababu.

TUJIUNGE NA CHANZO
Iliposambaa habari hiyo, mapaparazi wetu waliingia kazini kuchimba zaidi ubuyu huo ambapo walifanikiwa kuzungumza na mmoja wa marafiki wa Wema ambaye alieleza siri ya wawili hao kumwagana.

“Kilichomfanya Wema amwagane na Idris si kingine ni shilingi milioni 98. Unajua Madam anadaiwa fedha hizo ili alikomboe lile gari lake (Range Rover Evoque) linaloshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Sasa akamuomba Idris amlipie, jamaa akazingua. Hapo ndipo penye sababu kubwa iliyomfanya Wema amaindi hadi wakamwagana na Idris,” alisema shosti huyo wa Wema.


IDRIS ADAIWA KUFULIA
Akaendelea: “Nasikia Idris kwa sasa amefulia. Zile shilingi milioni 500 alizoshinda kwenye Shindano la Big Brother (Hotshot 2014) zote zimeyeyuka. Ameshindwa kumhudumia Madam, Wema ameona isiwe tabu, bora amuweke pembeni aangalie ustaarabu mwingine.”

GARI LILIVYOKAMATWA
Mapema mwaka huu, Wema akiwa katika mizunguko yake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar, alikamatwa na maafisa wa TRA waliokuwa wakifanya ukaguzi wa magari ambapo mrembo huyo alipotakiwa kuonesha vibali vya gari hilo ambalo awali alidai amejizawadia kwenye bethidei yake, hakuwa navyo na hata alipopewa muda wa wiki moja kuviwasilisha, hakuweza kufanya hivyo.
Baadaye, gari hilo lilishikiliwa na TRA ambapo walipoona Madam ameingia mitini, walianza kulinadi kwa shilingi milioni 98 hivyo mrembo huyo aliposikia, alimuomba Idris amlipie lakini jamaa inadaiwa alidunda.

SABABU NYINGINE
Chanzo kingine kilicho karibu na wawili hao kililieleza Amani kuwa mbali na shilingi milioni 98, sababu nyingine ambazo ni chanzo cha wawili hao kumwagana ni:

YA PILI
“Wema alikuwa hataki kufuatiliwafuatiliwa katika uhusiano wao. Kuna wakati Idris alizidisha kumfuatilia. Ilikuwa akimkosa kwake na kwenye simu, anamfuata kwa marafiki zake. Hata akijibiwa hayupo bado alikuwa anakwenda kwa rafiki husika kumtafuta.
“Kama mnakumbuka kuna kipindi alikuwa anakwenda kumfuata Wema hadi nyumbani kwa Aunt (Ezekiel). Sasa Madam ile kitu alikuwa hapendi.”

YA TATU
“Idris aligeuka kuwa tegemezi kwa muda mrefu. Wema mwanzoni hakushtukia, alitoa akiamini mapenzi ndivyo yalivyo lakini suala hilo lilipozidi nalo liligeuka kuwa kero. Wema anapenda akiwa na mtu kwenye uhusiano awe anamwagiwa mapesa kama vile ilivyokuwa kwa yule kigogo wake CK au Diamond.

YA NNE
“Sababu nyingine ni Idris kumzuia Wema kufanya matanuzi. Wema anataka akiwa nazo atumie sasa jamaa alipojifanya anajua kumpangia matumizi nalo lilikuwa tatizo. Madam unaanzaje kumbana kimatumizi kwa mfano?”

YA TANO
“Idris naye alimuona Wema kuhusu tukio lake la kupigana mabusu na yule mwanaume asiyeeleweka. Sasa kitendo hicho hakikumfurahisha Idris, akamchana ‘live’ Madam.”…

WEMA ANASEMAJE?
Alipotafutwa kuhusu sababu za yeye kummwaga Idris, Wema hakutaka kuingia moja kwa moja badala yake alifunguka kwa kifupi kuhusu sababu ya kupiga picha akiwa anambusu mwanaume huyo hivi karibuni.

“Ha! Ha! Haa! Davto tunazinguana tu na ni  mshikaji wangu kitambo… watu walikuwa kwenye pati and (na) tulikuwa tuna have fun (tunafurahia).”

IDRIS HUYU HAPA!
Jumatatu iliyopita, Amani lilimpigia simu Idris lakini hakupokea, alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa Instagram (Insta direct) kumuuliza juu ya yeye kumwagana na Wema pamoja na kufulia hadi kushindwa kumlipia Madam shilingi milioni 98, alicharuka na kuamua kujibu hadharani katika ukurasa wake wa Instagram.

“Nashangaa mwandishi kuniuliza kuwa nimefulia wakati sasa hivi mimi nipo vizuri kweli kweli. Nilifulia zamani na si sasa.”

“…mliokuja na skendo za Idris kuishiwa mbona mmechelewa sana? Mnazileta stori sasa hivi  wakati hela zimerudi… miezi minne nyuma zilipoisha mlikuwa wapi?”
Hata hivyo, taarifa za kufulia kwa Idris, zilitua kwenye dawati la gazeti hili siku nyingi nyuma lakini mwenyewe amekuwa akiwakwepa waandishi wetu, hivyo kufanya habari hiyo isiandikike kwa sababu za kitaaluma na kiweledi kwa kuwa haikuwa na mzani (balansi).

TUMEFIKAJE HAPA?
Idris alikipokea kijiti cha penzi la Wema mara baada ya kurejea Bongo akitokea Afrika Kusini akiwa amejishindia kitita cha shilingi milioni 500 kupitia Shindano la Big Brother.
Kabla ya hapo, mrembo huyo alikuwa akimilikiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye walimwagana na mshikaji huyo kuanza kutoka na Zarina Hassan ‘Zari’, mrembo kutoka Uganda.

Chanzo:Global Publishers

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na badooo bibi bomba. Ulidhani maisha ya kuhongwa dili. Idriss big up. Huyo michirizi kishazoea kuuza nyapu ili a survive town. Kwa nyapu gani mpaka umlipe 98ml?!. Alikupiga changa la macho eti ana mimba. Hahaha mimbaa?! Si tungehama nchi...

    ReplyDelete
  2. Hana hata haya. Fanya kazi. Achana na maisha ya kusubiri wanaume wakuhonge. Waone ma miss waliopita. Wote wame make it kasoro wewe tu. Lakini laana na machozi ya wake na wapenzi wa watu. Lazima utaharibikiwa tu....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo mdogo wangu Wema ni mvivu sana na anapenda sana starehe mpaka akashindwa shule sasa kazi aijuayo ni biashara ya kuuza pale double mti, na alishawahi kusema ye mwenyewe hawezi kuwa na bwana mmoja ATAKULA WAPI?

      Delete
  3. kumuomba pesa mpenzi wako ni kawaida, sasa huyo Idriss alikuwa analala. kula. kutomba bure. kwahiyo Wema ahangaike amlishe yeye? wapumbavu wakumbwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We kweli ni kahaba uliye kubuhu, kwa faida gani uliyonaye mpaka akupe hiyo hela? K ziko kibao mtaani tena za bure na hivi mlivojazana duniani, kama yako mali kauze tuone kama utapata hata buku. Mwanamke mwenye akili ni yule anayewaza namna ya kusaidiana na mwanaume wake namna ya kuzalisha kipato, ila makahaba kama nyie mawazo kwa chupi.

      Delete
  4. umeharibikiwa wewe Anony 12.56 PM. kwa kuwa huna hata dume lilojaribu kukutongonza mnuka uchi. Wema yuko juu na pesa anazo ila kumlipia dume zima liwe linamwaga tuu big nooo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona asilipie kagari yake kama pesa anayo, wanawake wezangu fanyani kazi acheni kutegemea vya kupewa. Imagine huyo mtu akifa ghala utahamie kawa mtu mwingine matokeo yake ndio mnakufa na ukimwi, au ndio hivyo unavyo dai ajali kazini!!!! achaeni ujinga fanyeni kazi

      Delete
    2. Aache kumhonga mama yake aliyemzaa ahonge baiskeli ya taifa ha ha ha ndio maana mnaishia kuwa magumegume nyie wanawake. Wanaume wanaona kama takataka hamfai kupewa heshima ya mke, hela yote hiyo akupe kwani unajamba almasi wewe?

      Delete
  5. Hapo iddrisa umefanya la maana umpe milion 98 kwa kipi naamini hata mamako mzazi hujawahi kumpa kiasi hicho cha pesa kwa hilo umetumia akili

    ReplyDelete
  6. amefanya la maana au alikuwa hana. ni kula kulala buree katimuliwa kiaina.

    ReplyDelete
  7. kwa macho tu ya kawaida bila kuvaa miwani ako kavulana hakana ela hiyo so wema kama ulitoa ukidhani ipo siku utapokea umetapeliwa! huyo masai alishafulia kitambo!

    ReplyDelete
  8. Wema unawezaje kupanda magari ya kifahari wakati bili ya umeme na bili ya maji inakushindwa kulipa mpaka ukafukuzwa kwenye nyumba, shika adabu yako, watu ambao wanakupa hela ni hao watu wanakutombo ule ulale

    ReplyDelete
  9. TZ 98M kukomboa gari kwani Idris ni baba yako mzazi? Gosh badala ya kuwaza kununua kiwanja ujenge usitirike usifukuzwe usiku usiku kama digidigi nyumba za watu khaaaa kweli huyu demu ni mburula kama team zake. Umri wake umeenda sana ila hana chochote cha kujioneshea mafanikio yake, soo sad.

    ReplyDelete
  10. mmmmmh!shikamoo wabongo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad