kuvunjika Kwa Kundi TMK Wanaume Kulimuuzunisha Sana Jakaya Kikwete-Chege Afunguka

Msanii kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chingunda amefunguka na kusema kuvunjika kwa kundi la 'Wanaume TMK Familiy' kulimuuzunisha mpaka aliyekuwa Rais wa awamu ya nne ya Tanzania Mh. Jakaya Kikwete.

Akizungumza kwenye kipindi cha MKASI kinachorushwa na EATV Chege alisema kuwa Rais Kikwete aliwaambia kuwa amehuzunishwa sana na kitendo cha kundi hilo kuvunjika kwani alikuwa akiona jinsi ambavyo walikuwa wamefanikiwa kuteka nchi kwa burudani na vile ambavyo waliweza kutoa burudani ya nguvu na kufanya biashara ya nguo zao na jinsi wananchi walivyokuwa wakiwapa support.

Chege amedai hata yeye mpaka sasa anatamani sana kundi hilo liweze kurudi kama lilivyokuwa awali, kwani kuna vitu vingi ambavyo anavikumbuka vilikuwa vinafanyika enzi hizo.

"Kiukweli kabisa mimi mwenyewe na kila mtu anatamani kundi la TMK Wanaume Familiy lirudi kama zamani hata sasa, sababu kuna vitu tulikuwa tukifanya navikumbuka sana, na siamini kama kuna mtu ndani ya kundi lile ambaye hapendi hicho kitu kitokee. Kuna wakati mpaka tuliitwa na Rais Jakaya Kikwete ili aweze kutuweka sawa turudi kama zamani sema mwenzetu mmoja hakuweza kutokea" Alisema Chege.

"Kuna wakati tulikuwa tunaweza kupanda stejini ili show iweze kuisha lazima polisi waingilie kati, na kuna siku zingine kwa siku moja tulikuwa tunaweza kufanya mpaka show tatu sehemu tofauti tofauti yaani hapo tunabadili nguo tu na kupanda sehemu nyingine, kiukweli nakumbuka mambo kama hayo" Aliongeza Chege.
Mbali na hilo Chege anakiri wazi kuwa msanii Juma Nature na uongozi ndiyo walikuwa na tatizo lao ila yeye si chanzo cha kundi hilo kuvunjika kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodai kuwa mwanamke ndiye alikuwa chanzo kwa kundi hilo kuvunjika. Lakini mbali na hilo Chege pia amekiri kuwa Juma Nature ndiye alikuwa msanii mkubwa kwenye kundi hilo na yeye aliweze kuwaweka wao kwenye ramani ya muziki wa bongo fleva mpaka kufikia hatua ya kufanya vyema na kukubarika kwa jamii.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaani kwa nini wanamuziki wa kibongo wana beat mbaya kwenye you tube ndiyo maana hamfiki mbali hata kama mkienda kufanya shuuting South afrika, ukiona wakongo wana beat na sauti nzuri katika you tube, wabongo jirekebisheni

    ReplyDelete
  2. kuanzia leo nitawasikiliza wakongo tu sababu wana beat nzuri na sauti nzuri kwenye mtandao, juzi juzi koffi olomide alikuja kufanya show dar, na shoo yake nimeisikiliza sana katika you tubu na inayo sauti nzuri sana, unaweza kusikia sauti anayoimba, lakini wabongo huwezi sikia sauti wanayoimba katika you tube

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad