Lemutuz Kayasema Haya.....
lemutuz_nation Mr. Isaack Jana Arusha akirudishwa Rumande baada ya kushitakiwa na Serikali kwa kumtukana Rais Magufuli kwenye mitandao ya kijamii ....hapa ndipo ninapoilaumu Polisi na Serikali I mean huyu mtu kamtukana Rais juzi tu Jana tayari Mahakamani kwa nini iwe hivyo na kwa wananchi wa Kawaida? ....Sheria ipo now kama kuna njia rahisi ya kuwakamata hawa Cyber Abusers ni kwa nini wanapotukanwa Wananchi wa Kawaida inakuwa almost kama hamna Sheria wala uwezekano wa kuwakamata lakini akitukanwa Rais Mara moja wanapatikana? ....ndio maana ninasema na sisi Wananchi tusimameni tuhesabiwe tukatae hawa watu kutuvurugia amani kwenye Social Media .....tupambane nao hata kama itachukua muda mrefu lakini wapate ujumbe kwamba sio Wananchi wote tupo tayari kuwapa hiyo nafasi tutawatafuta na watafikishwa kwenye Sheria tu hata kama ni Miezi SITA au Mwaka wa kuwatafuta! - le Mutuz 34min
Mbona Raisi Mkapa alitukana wananchi hadharani kiwa wapimbavu. Je sheria ni tofauti.mshikeni basi naye
ReplyDeleteMbona Raisi Mkapa alitukana wananchi hadharani kiwa wapimbavu. Je sheria ni tofauti.mshikeni basi naye
ReplyDeleteHapa ndio ninapoamini sheria msumeno, ukiuchunguza msumeno namna unavyofanya kazi utagundua kwamba msumeno haukati kotekote kama tunavyoaminishwa, msumeno hukata kwa kwende mbele tu, ukirudi nyuma huwa unasafisha haukati kwa kurudi nyuma. Hivyo tubadilishe huu msemo, tuseme sheria ni kisu maana kinakata kwa kwenda mbele na kurudi nyuma.
ReplyDeleteNakubaliana na mawazo ya Le mutuz, mwalimu nyerere moja kati ya hotuba zake alikataa kuwaita watu wapumbavu, akawaita wajinga. Kwa sababu alielewa uzito wa neno MPUMBAVU, Katika kampeni za uchaguzi aliyekua mkuu wa nchi aliwaita wananchi WAPUMBAVU NA MALOFA, na ikaonekana nijambo la kawaida, muda mfupi baadae aliyekua waziri wa mambo ya ndani aliwaita polisi WAPUMBAVU akakamatwa na kuwekwa ndani, haukupita muda mrefu tena mbunge akamuita mkuu wa wilaya kuwa ni MPUMBAVU,akafunguliwa mashtaka na akapatikana na hatia na sasa anatumikia kifungo cha nje kwa muda wa miezi mitatu. Swali, hivi hizi sheria zinawabana baadhi ya watu na kuwaacha baadhi yao? kuna walio chini ya sheria na walio juu ya sheria. Ama kuna vigezo gani vinavyotumika kuwakamata watu wanaotoa lugha chafu na za maudhi? Na kuna vigezo gani vinavyotumika kutowakamata wanaotoa lugha chafu na za maudhi.
Mkuki kwa nguruwe,
ReplyDeleteMh!! Mungu tusaidie jamani.
ReplyDelete